EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, September 25, 2012

Hakimu Aburutwa Kortini Kwa Rushwa

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala Pamela Kalala (kushoto),akitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana,baada ya kusomewa shitaka la kuomba rushwa ya Shilingi milioni tatu. HAKIMU Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Pamela Kalala amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa mke wa mmoja wa washtakiwa aliokuwa akisikiliza kesi yao.
Hakimu Kalala alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana asubuhi na kusomewa mashtaka matatu ya kuomba rushwa ya Sh3 milioni na kupokea rushwa ya Sh900,000 kwa nyakati tofauti. Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Allen Kasamala alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Aloyce Katemana kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti Februari, mwaka huu.

Katika kosa la kwanza, Kasamala alidai kuwa mshtakiwa huyo aliomba rushwa ya Sh3 milioni kutoka kwa Josephine Omar ambaye ni mke wa mmoja wa washtakiwa katika kesi namba 703 ya mwaka 2008 inayohusu kujipatia fedha kwa njia zisizo halali. Kasamala alidai kuwa mshtakiwa alimwomba Josephine kiasi hicho cha rushwa ili kumshawishi ampendelee mumewe katika kutoa uamuzi wa kesi hiyo aliyokuwa akiisikiliza. 

Katika shtaka la pili, Kasamala alidai kuwa Februari, tarehe isiyofahamika, mshtakiwa alipokea rushwa ya Sh800,000 kutoka kwa Josephine na katika kosa la tatu, alidai kuwa Februari 6, mwaka huu mshtakiwa alipokea rushwa ya Sh100,000 kutoka kwa mwanamke huyo. Kasamala alidai kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo akiwa mwajiriwa wa Idara ya Mahakama kwa wadhifa wa Hakimu Mkazi. Alisema Kalala alitenda makosa hayo kinyume cha Kifungu cha 15 cha Sheria ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007. 

Hata hivyo, mshtakiwa alikana mashtaka yote na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Hakimu Katemana alimwachia mtuhumiwa huyo kwa dhamana, baada ya kutimiza masharti ambayo ni pamoja na kusaini bondi ya Sh1 milioni na kuwa na mdhamini mmoja anayefanya kazi katika taasisi inayotambulika, ambaye pia alisaini bondi ya Sh1 milioni. Hakimu Katemana aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 23, kwa ajili ya kutajwa. Mahakimu na rushwa Kalala anakuwa hakimu wa nne kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu kwa tuhuma za rushwa, katika kipindi cha miaka mitano. 
Desemba mwaka 2007, aliyekuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Jamila Nzota alipandishwa kizimbani katika Mahakama hiyo akituhumiwa kupokea rushwa ya Sh700,000. Nzota alikuwa akikabiliwa na tuhuma za kuomba rushwa hiyo kutoka kwa Mollel, aliyekuwa Mwakilishi wa Kampuni ya Amanarth Enterprises Ltd iliyokuwa na kesi ya madai namba 33/207 mbele yake, ili amsaidie. 

Katika kesi hiyo, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Hanzron Mwankenja (mstaafu kwa sasa), alimhukumu Nzota kwenda jela miaka kumi na moja kuanzia Mei 22, 2009, baada ya kupatikana na hatia katika makosa manne yaliyokuwa yakimkabili. Hata hivyo, Hakimu Mwankenja alisema mshtakiwa atatumikia adhabu zote kwa pamoja, hivyo alitumikia kifungo cha miaka mitatu jela. Nzota hakuridhika na hukumu hiyo na kupitia kwa Wakili wake, Majura Magafu alikata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, lakini katika hukumu iliyotolewa na Jaji Emilian Mushi, Aprili 30, 2010, alishindwa tena. Wengine ni aliyekuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Adolf Mahai, (2007) na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Ukonga, Ndovela Kihenga.
CHANZO CHA HABARI >>> www.mwananchi.co.tz

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate