IRENE MWAMFUPE JAMIIblog tunaomba wasanii wa kike bongomovie kutunza nidhamu nje na ndani ya kazi zenu.Mavazi ni kitu cha msingi sana mbele ya jamii yetu ya kitanzania.
Hapa Bidada anaona Mpoki anampotezea mda tu kwa pumba zake,anamsubili amalize afanye yake.
Hapa sasa akaanza kujiuliza Jinsi atakavyo mfunika Anty
Kila anavyoangalia umati Wazimu unampanda.Akaanza chojoa sasa.
Maama yangu mauno sasa yameanza.Ila bado hamjaona nyiee wait!
Wikenda hii palikua hapatoshi mjini morogoro.Ikiwa ni wiki tu kupita tangu Msanii wa bongo Movie maarufu Anty Ezekiel kupamba kurasa nyingi za mitandao ya kijamii na magazeti kwa picha yake iliyoonyesha nguo yake ya ndani,Na yeye kukili baadae kua ilikua ni pombe mpaka kuomba msamaha kwa mashabiki wake.Msanii mwenzake Wema Sepetu juzi mjini morogoro katika jukwaa la Serengeti Fiesta 2012 aliamua kumwaga mboga kabisa baada ya kuachia Makalio yake makubwa hadharani bila hata ya kujishtukia mbele ya Maelfu ya watu waliofulika uwanjani apo.
Hii itakua mara ya pili ambako awali akiwa apoapo mji kasoro bahari,mnamo mwaka juzi akiwa jukwaa moja na Diamond Wema akiwa amevaa kigauni cha pundamilia strech (Mvutiko) alikua na wakati mzuri huo kwani kivazi hicho kilikua kina panda mara kwa mara na yeye kugeuka ili watu waone vizuri.Hii inanikumbusha ule msemo usemao Sikio la Kufa Halisikii Dawa..Hakika ni jambo la aibu saana hasa ndani ya bongomovie.Anty alisema ni Pombe tu,sasa sijui yeye Wema atasemaje.
No comments:
Post a Comment