EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, September 20, 2012

MADEREVA PIKIPIKI WAANDAMANA NA KUFUNGA BARABARA MASAA MATATU POLISI WAWATAWANYA KWA MABOMU

Waandamanaji ambao ni madereva wa pikipiki mkoani Arusha,wakiwa wamefunga barabara ya Moshi Arusha katika eneo la Ngulelo huku wakionyesha moja ya mabango waliokuwa nao.
 Madereva wa bodaboda wakiziba barabara kuu ya Arusha Moshi na kufanya magari zaidi ya 100 kushindwa kupita kwa saa 3
 Askari wa FFU wakifyatua mabomu ya machozi kuwatawanya madereva hao waliokuwa wamefunga njia
Dereva pikipiki ambaye hakujulikana  mara moja jina lake akitaka kupasua kioo cha gari dogo baada ya dereva wa kagi hilo  kutaka kupita eneo walilosuia.
 
MADEREVA pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda zaidi ya 300,jijini hapa wameandamana na kufunga barabara kuu ya Moshi Arusha kwa zaidi ya saa 3 ,katika eneo Ngulelo jijini hapa , wakilituhumu jeshi la polisi kumwachia mtuhumiwa wa mauaji anayedaiwa kumuua kwa kumpiga risasi mwenzao bila hatia.
 
Madereva hao wakiwa na pikipiki zao, walifunga barabara hiyo kuanzia majira ya  saa 4  asubuhi hadi saa 6 mchana kwa mawe na magogo hali iliyolazimu jeshi la polisi kikosi cha kutuliza ghasia kuingilia kati na kuwatawanya kwa mabomu ya machozi na risasi za moto .
Kwa mujibu wa mmoja wa waendesha pikipiki,Jonathan Emanuel ,Mkazi wa Ngulelo wilaya ya Arumeru,maandamano hayo yalilenga kulaani mauaji ya mwenzao aliyemtaja kwa jina la Hilari Elias (36)mkazi wa Oldadai, aliyeuawa kwa kupigwa risasi  septembe 15 mwaka huu akiwa barabarani  eneo la baraa akimsafirisha abilia aliyekuwa amemkodi.
 
 
Madereva hao wakiwa na mabango  yenye ujumbe mbalimbali  wa kulaani jeshi la polisi kumwachilia mtuhumiwa wa mauaji(jina linahifadhiwa) anayedaiwa kuwa na uwezo wa kifedha na mmiliki wa garage ya kutengeneza magari  na mkazi wa Baraa jijini hapa ,walilituhumu jeshi la polisi mkaoni hapa kwa kucheza mchezo mchafu wa kumwachulia mtuhumiwa aliyempiga risasi dereva mwenzao na kumsababishia kifo chake.

Maandamano hayo yalianzia katika kituo cha basi eneo la Ngulelo majira ya saa 2 asubuhi kuelekea mjini katika chumba cha maiti katika hospitali ya mkoa Mount Meru kuuchukua mwili wa merehemu na baadaye yalielekea nyumbani kwa mtuhumiwa ambapo madereva hao kwa pamoja  walivunja lango la kuingilia na kuharibu mali za mtuhumiwa ikiwemo gari lake  lililovunjwa vioo vyote pamoja na vyoo vya nyumba hiyo.
 
Aidha baada ya tukio hilo madereva hao walifunga barabara katika eneo la Ngulelo kwa mawe na magogo wakishinikiza  mkuu wa mkoa wa Arusha ,Magesa Mulongo kufika eneo hilo na kuwasikiliza kwani walikuwa hawana imani na jeshi la polisi huku wakidai ya kuwa mtuhumkiwa wao naonekana akirandaranda mitaani.
 
Katika eneo hilo pamoja na kufunga barabara hiyo,madereva hao  walivunja vioo vya magari kwa kupiga mawe vioo vya magari na kuharibu baadhi ya magari yaliyokuwa yakijaribu kupita kwa nguvu wakati wamefunga barabara hiyo,huku wakipaza sauti kwa kupiga yowe wakiwa wamelala barabarani huku wakitaka mkuu wa mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo afike kuwasikiliza kilio chao kwani hawana imani na jeshi la polisi.
 
Hata hivyo polisi baada ya kufika eneo la tukio, waandamanaji hao walianza kupiga yowe huku wakirushia mawe  gari la polisi ambao walilazinika kuondoka kwa kasi kwa lengo la kujinusulu, ambapo baadae walirejea wakiwa na nguvu mpya  na kuanza kuwafyatua mabomu zaidi ya 10 na kufanikiwa kuwasambaratisha na kufungua njia .
 
Akisimulia chanzo cha mauaji hayo,Jonathan Emanuel alieleza kuwa siku ya tukio marehemu akiwa na dereva mwenzake walikodishwa na abilia  wawili kwa lengo la kuwapeleka nyumbani kwao,lakini wakiwa njiani waliliona gari aina ya Escudo kwa mbele yao na kujaribu kulipita.
 
Alisema kuwa marehemu alijaribu kulipita gari hilo lakini  dereva wa gari hilo ambaye ni mtuhumiwa alimzuia kwa kuziba na kusimama ambapo alimuuliza alikuwa anakimbilia wapi.
‘’huyo dereva wa escudo alimzuia marehemu kupita kwa kuziba njia na kumhoji kuwa kwanini anakimbia na alikuwa nakimbilia wapi’’alisema
 
Alisema kuwa kulitokea majibishano  baina ya marehemu na mtuhumiwa ndipo mtuhumiwa huyo alipochomoa bastola na kumfyatulia risasi kifuani na kufariki dunia papo hapo huku abilia wake akiduwaa asijue la kufanya.
 
Madereva hao wanadai kuwa jeshi la polisi mkoani Arusha wameshindwa kuwatendea haki kwa kumbana mtuhumiwa ambaye anaonekana mtaani huku akitamba kuwa yeye ni zaidi yao na kwamba hawezi kufungwa kama wanavyofikiria.

Tukio hilo limethibitishwa na kamanda wa polisi mkoani Arusha,Liberatus Sabasi na kueleza kuwa polisi bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na kuahidi kulitolea ufafanuzi hapo baadae,na mwili wa merehumu huyo umezikwa na umati mkubwa wa watu nyumbani kwap en o la Oldadae.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate