Ndani ya uwanja wa Karume
mjini Musoma,wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2012 lilipokuwa
linaunguruma usiku wa kuamkia leo.
Msanii
wa filamu Bongo, Vincent Kigos 'Ray',akionesha manjonjo yake kwenye
tamasha la Serengeti Fiesta 2012, muda mfupi baada ya kukaribishwa kwa
ajili ya kuwasalimia baadhi ya mashabiki zao waliokuwa wamefurika ndani
ya uwanja wa Karume mjini Musoma.
Msanii
mwenye umbo kubwa katika tasnia ya filamu Bongo, Jacob Steven 'JB',
akionesha uwezo wa kunengua kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012
ndani ya uwanja vya Karume mjini Musoma.
Kati
ya mashabiki waliyoshindwa kujizuia katika tamasha la Serengeti Fiesta
2012, wakizungusha nyonga zao kama inavyoonekana kwenye viwanja vya
Karume mjini Musoma.
Ray
na Steve Nyerere (wa kwanza kutoka kushoto), wakishindana kusakata
sebene kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya uwanja wa Karume
mjini Musoma.
Ray akipagawa na jukwaa huku makelele yakiwa yametawala kila kona uwanjani hapo.
Rais
wa masharobaro Bongo, Bob Junior (katikati), akisongesha burudani za
Serengeti Fiesta 2012, na Wanenguaji wake ndani ya Viwanja vya Karume
mjini Musoma.
Ommy Dimpoz akipagawisha mashabiki wake ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma, katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Mwasiti
akiwa amepakatwa na mmoja wa mashabiki zake kwenye Tamasha la
Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma huku
akiyamwaga mauno ya kiuchokozi chokozi.
Mmoja
wa wasanii waliyoibuka kidedea katika mchakato wa Serengeti Super
Nyota 2012, akidhihirisha uwezo wake wa kuimba ndani ya uwanja wa
Karume mjini Musoma.
Chege,Temba na Bi Cheka wakiwajibika jukwaani kwenye onesho la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma.
Mashabiki wa kizungu wakipagawa na burudani ya Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini msoma.
Baadhi ya sehemu ya umati wa mashabiki waliozama ndani ya viwanja hivyo wakishuhudia burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.
Mashabiki wa burudani za Serengeti Fiesta 2012, wakiwa wamefurika uwanjani hapo tayari kwa kushuhudia burudani mbalimbali.
No comments:
Post a Comment