Na Shakoor Jongo -- Chende ‘Dogo Janja’ (15), anadaiwa kutembea mitaani akiwa na bastola wakati umri wake hauruhusu kumiliki silaha hiyo kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mtoa taarifa aliyeshuhudia habari hii anasema kuwa ni hatari kwa kijana huyo kutembea na bastola ambayo inasemekana si mali yake na kama vile hiyo haitoshi, huwa anaonekana nayo maeneo ya Coco Beach, Masaki, Dar es Salaam.
Lawama nyingi zilielekezwa kwa Mkurugenzi wa Mtanashati Entertainment, Ostaz Juma na Musoma ambaye ndiye anayemlea Dogo Janja na kusimamia kazi zake.
Ostaz Juma alipoulizwa kuhusu suala hiyo, alisema kuwa bastola hiyo si mali yake bali ni ya jamaa mmoja ambaye ni promota maarufu mkoani Dodoma.
Dogo Janja alipohojiwa, alikiri kushika bastola na kupiga nayo picha.
GlobalPublishers.info
No comments:
Post a Comment