MWIGIZAJI wa filamu mwenye jina kubwa Swahiliwood Amanda Poshy amefunguka kuhusu kutalikiana na aliyekuwa mumewe Hamis Bwela ambaye aliachana naye siku za karibuni kutokana na sababu ya mumewe kumzuia asifanye kazi yoyote zaidi ya kukaa ndani tu na kama akitoka wawe sote.
Amanda Poshi mwigizaji wa filamu Swahiliwood.
“Ndoa imenishinda aliyekuwa mume wangu alikuwa hataki kabisa nifanye kazi yoyote zaidi
ya kukaa ndani tu, maisha ya sasa si maisha ya kusubiri uletewe kila kitu lazima mwanamke uhangaike na si kuwa tegemezi sasa mtu ukae ndani tu kama mwali au mwanamke wa mwarabu maisha ya sasa,”anasema Amanda.

Amanda Poshy katika pozi.
Amanda amedai kuwa mumewe alipomuoa alijua kuwa yeye ni mwanamke mjasiriamali ambaye pamoja na kufanya shughuli zake ndogo ndogo lakini kazi yake kubwa ni uigizaji ambayo anaamini kuwa inawezekana hata mumewe huyo alimwona kupitia filamu na tamthilia na kumpenda awe mkewe iweje amzuie asifanye kazi yoyote?
No comments:
Post a Comment