Salma Jabu ‘Nisha’.
Nay wa Mitego
SALMA Jabu ‘Nisha’ anayefurukuta kwenye tasnia ya filamu Bongo, ameibuka na kunadi uhusiano wake na msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kwamba mambo yamekwiva na muda wowote atavutwa ndani.
Huyu hapa Nisha: “Mimi na Nay wangu sasa mambo safi. Muda wowote mnaweza kusikia mengine. Mama yangu amemkubali na amempokea kwa mikono miwili. Kikubwa alikuwa hataki kusikia natoka na mume wa mtu.
“Ameridhia kwani hachagui kabila wala dini ilimradi awe siyo mume wa mtu. Kwa sasa Nay yupo kwenye shoo za Fiesta, akimaliza tutaanza taratibu za ndoa.”
No comments:
Post a Comment