Rais Jakaya Kikwete akiweka
saini kitabu cha maombolezo ikulu ya Addis Ababa jana, kufuatia kifo cha
Waziri Mkuu wa Ethiopia marehemu, Meles Zenawi anazikwa leo. Wengine
katika picha ni baadhi ya wajumbe waliofuatana na Rais Kikwete
watakoshiriki mazishi ya kiongozi huyo. Kutoka kushoto ni, Livingstone
Lusinde, Aliyewahi kuwa balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Jenerali
Mirisho Sarakikya, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Joram Boswaro,
Zitto Kabwe na Waziri wa Kazi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,
Haroun Ali Suleiman. (Picha na Freddy Maro)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiweka shada la maua na kutoa heshima zake mwisho kwa aliyekuwa Waziri
Mkuu wa Ethiopia Marehemu Meles Zenawi katika ikulu ya Addis Ababa leo
jioni (Picha na Freddy Maro)
No comments:
Post a Comment