MMOJA wa wadhamini wa shindano hili ambao ni kampuni bab’ kubwa inayodili na uuzaji wa urembo na vipodozi vya wanawake ya Shear Illusions, imetangaza zawadi nono kwa atakayeibuka mshindi.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Shekha Nasser akizungumza na Showbiz alisema mrembo atakayeshinda atapewa ofa ya kufanya bonge la shopping katika moja ya maduka yao.
“Kama tulivyoahidi mshindi tutampa ofa ya kuja kufanya shopping kubwa lakini pia nichukue fursa hii kuwataarifu wanawake wote kuwa, siri ya urembo wa mastaa wengi na wanawake wanaoonekana wana mvuto ni Shear Illusions hivyo watembelee maduka yetu yaliyopo Kibo Tower -Tegeta, Millennium Tower-Kijitonyama na Mlimani City kwa jijini Dar,”alisema Shekha.
Wasomaji wanatakiwa kuendelea kupiga kura kumchagua mshindi na wiki ijayo atatangazwa kupitia ukurasa huu. Ili kushiriki katika kumchagua mshindi kati ya Wema na Agnes, andika jina la anayestahili kutoka kisha litume kwenda namba 0786799120.
No comments:
Post a Comment