Uongozi
wa Shule ya Sekondari ya Majengo, Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro
inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi umeridhia kuacha kazi
kwa mwalimu wa kiume wa shule hiyo anayedaiwa kujihusisha na mapenzi ya
jinsia moja.
Kufuatia hatua hiyo, Bodi ya shule
imemlipa mwalimu huyo Endrew Katto, Sh. 2,409,924 kama kiinua mgongo
baada ya kuitumikia shule hiyo kwa miaka sita.
Mwalimu Katto aliajiriwa katika shule hiyo
Februari Mosi, 2006 hadi Februari Mosi mwaka huu, alipoamua kuandika
barua hiyo na kumfungulia kesi Mkuu wa shule hiyo, Bruda Peter Lyimo,
kwa madai ya kumtukana kwa maandishi katika kituo kikuu cha polisi Mjini
Moshi na kufungua jalada Na. MOS/RB/11709/2012
Alipotakiwa na NIPASHE kueleza sababu za
kuandikiwa barua hiyo alisema hawezi kuzungumzia kwa undani kwa kuwa
alishamuelekeza wakili wake kuchukua hatua za kisheria
Aidha, mwalimu huyo amewasilisha barua ya
kutaka aombwe radhi na kulipwa fidia ya Sh milioni 800 kupitia wakili
wake Kipoko & Advocate, akidai kuwa Bodi ya shule imemdhalilisha na
kuchafulia jalada la taaluma yake hali inayomsababishia asiajiriwe
sehemu yoyote.
Hata hivyo, wakili huyo aliiambia NIPASHE
kwa njia ya simu kuwa endapo watamuomba radhi mteja wake na kumlipa
gharama na kuridhika hawataenda mahakamani
Kwa mujibu wa barua ya Mkuu wa shule hiyo,
Bruda Peter Lyimo ya 18/04/2012 yenye kumbukumbu Na. MSS/PP/AK/189/30
imeeleza kuwa uongozi wa shule umeridhia mwalimu huyo kuacha kazi baada
ya kubainika kuwa alikuwa akijihusisha na masuala ya kujamiiana kinyume
cha maumbile.
“The school administration received your
letter dated 12.04.2012 in which you clearly stated that you will not
keep on working at this shool as a teacher after a homosexual scandal
was revealed on you” (Utawala wa shule umepokea barua yako ya tarehe 12.
04. 2012 ambayo umeeleza wazi kuwa huwezi kufanyakazi katika shule hii
kama mwalimu baada ya kubainika kwa kashfa dhidi yako ya kujihusisha na
mapenzi ya jinsia moja),”
ilisomeka sehemu ya barua hiyo ikimaanisha kuwa kuacha kazi kwa mwalimu huyo kulitokana na kubainika kushiriki suala la ushoga.
Akizungumza na NIPASHE ofisini kwake,
Bruda Lyimo alikiri kuandika barua hiyo kwa maelezo kuwa aliiandika
akiwa makini kwa kuwa ushahidi upo nakuongeza kuwa Majengo Sekondari ni
shule inayoheshimika nchini kwa elimu na malezi bora kwa hiyo sio busara
kuendelea kuwa na mwalimu aliyekiri kuwa ni shoga.
Habari zilizolifikia gazeti hili na
kuthibitishwa na Mkurugenzi wa Elimu Jimbo Katoliki la Moshi, Padre
Wiliamu Ruaichi, zimeeleza kuwa uongozi wa kanisa hilo bado unatafakari
hatua iliyochukuliwa na bodi.
CHANZO:
NIPASHE JUMAPILI
utafakali nini wakati huyu bwana ni shoga? mi namjua tangu primary kule Mlimani ile shule ya msingi iliyopo chuo kikuu cha dar es salaam? Alienda st.Antony mbagala nako vilevile, Tambaza sekondary ndio kabisa ikawa sio kificho tena hadi wakati yupo UDSM kusomea education alikua vilevile Agape secondary alikua akiwapa wanafunzi deiwaka, mke wake mwenyewe kamkimbia kwa sababu alimfumania akiwa na mwanafunzi wa kiume chumbani hadi mdada wa watu akakimbilia kwao kujiuliza kwanza. Shule isiombe radhi wala nini lazima maadili yazingatiwe yule ni shoga mzoefu tu hawamsingizii hata kwao kimara baruti kule wanamjua wakaulize baba yake mwenyewe marehemu mzee Kato alikua akimtukana kila uchwao kuhusu tabia zake hizo bahati mbaya sababu ya ugomjwa alishindwa kumwadhibu
ReplyDelete