EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, September 16, 2012

Tanzania ina wanachama hai zaidi ya 600 Freemasons

Tanzania ina wanachama hai zaidi ya 600 wa kundi la watu wenye imani ya siri ya Freemasons wakiwa wanatokana na watu wa kada mbalimbali wakiwemo maarufu, huku ikielezwa kwamba miongoni mwao hakuna viongozi wakuu wa serikali.

Hayo yalibainishwa na Kiongozi wa kundi la Freemasons katika eneo la Afrika Mashariki, Jayantilal Keshavji Chande maarufu kama Sir Andy Chande alipozungumza na gazeti hili (HabariLeo), wiki hii Dar es Salaam.

Kiongozi huyo Mtanzania mkazi wa Dar es Salaam mwenye asili ya Kiasia, alisema licha ya Tanzania kuwa na wanachama hao, kwa sasa idadi ya wanachama duniani inapungua tofauti na inavyoonekana sasa kuwa wanaongezeka kutokana na kuibuka maneno mengi kuhusu kundi hilo.

Alisisitiza kuwa si rahisi kumjua mwanachama wa kundi hilo, bali wenyewe ndio wanaofahamiana, akisema ni siri na kwamba wenyewe wanakutana katika vikao mbalimbali mara moja kwa mwezi au zaidi.

Alisema nchini kuna wanachama wakiwemo wafanyabiashara, watumishi serikalini, walimu pamoja na wanataaluma mbalimbali wanaoheshimika sana na kusisitiza kuwa kuna maneno mengi yanayosemwa kuhusu kundi hilo, ambayo siyo ya kweli. Alisema idadi ya wanachama wake duniani inazidi kupungua kutoka milioni nane hadi sasa wako milioni sita, tofauti na wengi wanaodhani kuwa idadi hiyo inaongezeka.

Chande alizungumza na mwandishi wa habari hizi katika Shule ya Sekondari ya Shaaban Robert ambako yeye ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule alipozungumzia maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake, alisema duniani kuna watu wazito wengi ambao ni wanachama wa kundi hilo kama majaji wakubwa na hata Binamu wa Malkia Elizabeth wa Uingereza ni kiongozi mkubwa wa kundi hilo.

Akizungumzia masharti ya kujiunga na kundi hilo, Chande alisema ni lazima mwanachama huyo awe anaamini katika Mungu bila kubagua iwapo ni Mkristo au Muislamu.

Alisema pia ni lazima anayetaka kujiunga awe na umri unaozidi miaka 21 na walio chini ya umri huo hawaruhusiwi kujiunga na lazima familia ya anayetaka kujiunga na wanandugu wafahamu kuwa umejiunga na kundi hilo.

“Unajua katika imani hii kuna michango mbalimbali ambayo unatakiwa kutoa ambayo ni zaidi ya dola milioni sita (karibu Sh bilioni 10), hivyo ni lazima ndugu wafahamu ili kuepuka matatizo utakapotakiwa kutoa,” alisisitiza.

Alisema si kweli kuwa wenye fedha wengi ni wanachama wa kundi hilo huku akikanusha wanachama wanajiunga kwa ajili ya kupata fedha, bali ni dini kama imani nyingine. Alisisitiza kuwa hakuna ukweli kwamba wanaopata mafanikio katika maisha wakiwa ndani ya imani ya Freemasons kuwa wanatoa kafara watu wao wa karibu kwa lengo la kupata utajiri.

Chande pia alisema hairuhusiwi kutumia jina la kundi hilo kwa nia ya kujipatia nafasi sehemu mbalimbali au kuongeza nafasi katika chuo au shule.

via HabariLeo

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate