EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, September 17, 2012

Watanzania waishio Afrika Kusini wakamatwa JKNIA na fedha bandia Euro Milioni 10


Na Willbroad Mathias, Majira, Dar es Salaam -- JESHI la Polisi Kikosi cha Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, kinawashikilia Watanzania wawili waishio nchini Afrika Kusini baada ya kukamatwa wakiwa na Euro bandia zenye thamani inayokadiliwa kufikia sh. milioni 10.

Vyanzo vyetu vya habari vimedai kuwa, watuhumiwa hao ni mwanamke na mwanaume ambao walikamatwa juzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JKNIA), Dar es Salaam.

Inadaiwa kuwa, kabla ya kukamatwa ulitokea mvutano kati ya mtuhumiwa mwanamke na mwenzake ambaye waliambatana katika uwanja huo wakati mtuhumiwa mwanaume akiwa ndani. Hali hiyo iliwafanya polisi kuingiwa na shaka hivyo walianza kufuatilia kile kinachobishaniwa.

“Kabla ya kuwakamata watuhumiwa, ulitokea mvutano wakati huo mtuhumiwa wa kiume alikuwa katika chumba cha mapumziko tayari kwa safari ya kwenda nchini Afrika Kusini. Baada ya polisi kubaini chanzo cha mabishano hayo, waliamua kumsaka mtuhumiwa wa kiume na kumfanyia upekuzi upya ndipo alipokutwa na Euro bandia,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa, mbali ya kukamatwa na Euro hizo mtuhumiwa huyo pia alikutwa na fedha nyingine za Kitanzania zinazokaribia kufikia sh. milioni tatu pamoja na hati mbili za kusafiria moja ya Tanzania na nyingine Afrika Kusini.

Akithibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao, Kamishna Mkuu wa Kikosi hicho, Kamanda Ulrich Matei, alisema walikamatwa saa tisa alasiri na kuwataja majina yao kuwa ni Bw. Omary Salum na Bi. Khadja Yusuf, ambao wanaishi nchini Afrika Kusini. Alisema kwa mujibu wa maelezo ya Salum, alikuja ili kununua dhahabu na kopa mjini Songea, mkoani Ruvuma, lakini baada ya kufika mkoani humo alikuta biashara ni ngumu akaamua kuondoka. Aliongeza kuwa, Salum baada ya kufika Dar es Salaam, alikuwa apokelewe na Yusuf, ambaye kwa sasa yupo Tanzania lakini anaishi nchini humo. Hata hivyo, Kamishna Matei alisema baada ya kuhojiwa, Salum alidai fedha hizo alibadilishana na raia mmoja wa China ambapo yeye alimpatia randi 70,000 na kupewa kiasi hicho cha fedha.

Akizungumzia mazingira yaliyosabisha kukamatwa kake, Kamanda Matei alisema siku ya tukio Salum alikuwa akutane na Bi. Yusuf, uwanjani hapo, “Bw. Salum alipofika uwanja wa ndege, mwenyeji wake Bi. Yusuf alikuwa amechelewa, muda wote walikuwa wakiwasiliana kwa simu ya ofisa wetu mmoja kwani mtuhumiwa hakuwa na laini ya simu za Tanzania,” alisema Kamanda Matei na kwamba baada ya muda mfupi, Bi. Yusuf aliwasiri uwanjani hapo akiwa na mwanamke mwingine aliyemtaja kwa jina la Bi. Zamzam Shaban.

Bi. Shaban aliuliza alipo Salum na baada ya kuambiwa tayari ameingia ndani, alianza kulalama na kudai mtuhumiwa alikuwa mpenzi wake na walikubaliana ampe pesa badala yake amemtoroka hivyo aliamua kutoa siri ya mtuhumiwa kufanya biashara ya kuuza noti bandia.

Alisema hivi sasa wanamshikilia Bi. Yusuf kwa sababu baada ya Bi. Shaban kutoa siri hiyo, alituma ujumbe mfupi (sms), kumjulisha Bw. Salum kuwa atafute njia ya kujinusuru.

Ujumbe huo ulitumwa katika simu ya ofisa huyo baada ya Bi. Yusuf kudhani kuwa, simu hiyo ilikuwa ya mtuhumiwa ambapo kazi ya kumsaka Bw. Salum, ilianza na kukamatwa.


No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate