Kocha Mkuu wa Yanga Tom Saintfiet (kushoto) akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu leo, kulia ni Katibu Mkuu Mwesigwa Selestine. (Picha na Mahmoud Zubery).
Kocha mkuu wa Young Africans Sports Club Tom Saintfiet ametengaza kikosi cha wachezaji 22 wataokondoka kesho alfajiri kuelekea jijini Mbeya tayari kwa ajili ya mchezo wa ufunguzi wa ligi Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons Septemba 15 siku ya Jumamosi.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Saintiet amesema ana kikosi kizuri cha wachezaji 30 lakini kutokana na katika mchezo kuitajika wachezaji 18 watakao vaa, amaeona ni bora kwenda na wachezaji 22 tu.
Saintfiet amesema wachezaji wanaobakia Dar es Salaam sio kwamba hawana uwezo, bali amechagua wachezaji kulingana na nafasi, nidhamu na uwezo binafsi wa mchezaji katika nafasi anayocheza.
Wachezaji ambao hawatasafiri na timu kwenda Mbeya, wataendeela kufanya mazoezi na kikosi cha U-20 mpaka hapo timu itakaporejea siku ya Jumapili jioni na siku ya Jumatatu wataendeela kufanya mazoezi pamoja.
Timu itaondoka kesho alfajiri kueleeka jijini Mbeya ambapo inatazamiwa kufika mida ya jioni saa 11 mpaka saa 12, wachezaji watapumzika na siku ya Ijumaa jioni watafanya mazoezi katika uwanja wa Sokoine kabla ya mchezo wenyewe siku ya Jumamosi.
Tunakwenda Mbeya kwa lengo la kurudi na pointi 3, najua Mbeya wamekuwa hawana timu ya ligi kuu kwa muda hivyo watacheza kwa nguvu kuhakikisha wanatoa upinzani, ila kwa kuwa Yanga ni timu bora Tanzania na Afrika Mashariki naamini tutashinda na kurudi na pointi 3 muhimu.
Wachezaji wataondoka kesho kuelekea Mbeya ni:
Walinda Mlango: Yaw Berko na Ally Mustapha 'Barthez'
Walinzi wa Pembeni: Shadrack Nsajigwa, Juma Abdul, Godfrey Taita, Oscar Joshua, David Luhende na Stephano Mwasika
Walinzi wa Kati: Mbuyu Twite, Kelvin Yondani na Nadir Haroub 'Cannavaro'
Viungo Wakabaji: Athuman Idd 'Chuji' na Frank Domayo
Washambuliaji wa Pemebeni: Shamte Ally na Saimon Msuva
Viungo Washambliaji: Haruna Niyonzima, Nizar Khalfan na Rashid Gumbo
Washambuliaji: Said Bahanunzi, Hamis Kiiza 'Diego', Jeryson Tegete na Didier Kavumbagu
Aidha kocha Saintfiet amesema anajua uwanja wa Mbeya ni mbovu, hauko katika kiwango kizuri na ndio maana wiki hii yote aliamua kufanya mazoezi katika uwanja wa Mabatini Kijitonyama ili kuzoea hali mbaya ya uwanja wa Sokoine.
Wachezaji wanaobaki ni:
Said Mohamed, Ladislaus Mbogo, Ibrahim Job, Salum Telela, Omega Seme, Nurdin Bakari, Idrisa Rashid, Juma Seif 'Kijiko' na Isa Hamis Ngao (U-20).
NB:Rekodi ya kocha Tom Saintfiet tangu ametua Yanga amecheza mechi 12, ameshinda 11 na kufungwa mchezo 1.
Chanzo: www.youngafricans.co.tz
No comments:
Post a Comment