Mabingwa wa Afrika mashariki na kati, klabu ya Yanga ya Dar es Salaam leo hii imekula kichapo mabao matatu kwa nunge kutoka kwa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Manungu mjini Morogoro.
Kipindi cha pili Yanga wakafanya mabadiliko kwa kuwaingiza Saimon Msuva na Stephano Mwasika kuchukua nafasi za Frank Domayo na David Luhende lakini haikusadia chochote. Dakika ya 66 akatoka Mbuyu Twitte na kuingia Didier Kavumbangu lakini mambo yaliendelea kuwa magumu kwa upande wa watoto wa Manji.
Dakika ya 77 ya mchezo alikuwa yule yule Juma Javu akaenda kumtungua golikipa Ally Mustapha Barthez goli 3 na la mwisho katika mchezo huo. Dakika ya 90 Yanga wakapata penati lakini Hamis Kiiza akashindwa kufunga na mwamuzi akapuliz kipenga cha kuashiria mwisho wa mchezo.
No comments:
Post a Comment