Mshindi wa OUT Miss Excellence 2012 Zuena Naseeb akitabasamu kwa furaha baada ya kunyakua taji hilo katika mashindano yaliyofanyika katika ukumbi wa Mwinyi Kinondoni Biafra. Kulia ni mshindi wa pili Naima Julius na kushoto ni mshindi wa tatu Tela Alestas.
Mgeni rasmi katika shindano la ulimbwende la OUT Miss Excellence 2012 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera (Mb) Kulia akimkabidhi mshindi wa kwanza mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 6 na Elfu Thalathini (6,030, 000/-) itakayo muwezesha kusoma ‘masters’ katika Chuo kikuu Huria cha Tanzania. Kushoto Profesa Tolly Mbwete.
Warembo waliofanikiwa kuingi katika Tano Bora kwenye mchuano wa OUT Miss Excellence 2012.
Meza Kuu ya Majaji wakifanya tathmini.
Mamiss wakitoa burudani kabla ya kuanza kuchuana katika OUT Miss Excellence 2012.
Kazi ya kupita mbele ya majaji na vazi la kutokea ikaanza rasmi.
Haya sasa ni vazi la ufukweni.
Mwanamuzi anayekubalika hapa nchini Banana Zorro akiimba kwa hisia wakati akitoa burudani kwa washiriki na wageni katika mashindano ya ulimbwende ya OUT Miss Excellence 2012.
Via dewjiblog.com
No comments:
Post a Comment