Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam wamekutana na kutoa tamko la kuzuia Waislamu kuacha kuandamana mara moja.
Katika taarifa ya waliyoitoa mapema leo asubuhi wakuu na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo wa dini wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadick, aliwatoa hofu wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwani wamejipanga kulinda hali ya amani.
Akitoa tamko hilo, Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa kumekuwapo na taarifa za waumini wa Kiislamu kuandamana na kufanya fujo mara baada ya swala ya Ijumaa na baadala yake amewataka kuacha kufanya hivyo na warejee majumbani kwa amani na suala hilo linashughulikiwa kisheria.
Hata hivyo kwa upande wao viongozi wa dini waliokutana na Mkuu wa mkoa juu ya kutolea tamko hilo waliwaasa waumini wote kutoingia mitaani na kuandamana kwani wakifanya hivyo ni kukiuka misingi mbalimbali ya kisheria iliyopo kihalali na watakapofanya hivyo ni kukiuka sheria za nchi.
Kamanda Kova, Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Musa bin Salum amewataka wakuu wa misikiti mkoa wa Dar es Salaam kuwakataza waumini hao kufanya maandamano kwani kufanya hivyo ni kukiuka misingi iliyopo. Aidha, aliwaomba waumini warejee majumbani kwa amani.
Askofu Makunda aliwataka watanzania kuendelea kufuata misingi ya kiimani bila chuki wala kufanya fujo.
Kamanda wa Polisi Kanda maalum mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova alitoa onyo kali kwa waislamu kuacha kufanya hivyo hii leo kwani kwa atakaekiuka atachukuliwa hatua kali. Kova aliwataka waumini kurejea majumbani mwao kwa amani bila kufanya maandamano na pia aliwataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuendelea na shughuli zao kama kawaida na kupuuza tishio hilo la fujo kutoka kwa waislamu.
“Jeshi limejipanga kuakikisha hali ya amani na usalama inakuwepo hivyo taadhari kwa waislamu kuacha kufanya maandamano mara moja” alisema Kova kwenye kikao hicho ambacho kinaendelea hivi sasa.
Wakuu hao wamekutana kwa dharura baada ya kuwepo kwa taarifa za juu ya waumini hao kutishia kuandamana na kufanya fujo.

Kariakoo (picha: Janeth Stephano via facebook.com)
DAR ES SALAAM, Tanzania
Vurugu kubwa zimetokea mchana huu katika maeneo yanayozunguka eneo la Kariakoo na kusababisha hofu kubwa na Polisi wamelazimika kutumia mabomu ya machozi na kutawanya mikusanyiko ya watu waliokuwa wamejiandaa kuandaamana kuelekea katika Ikulu ya Magogoni jijini.
Maduka yote katika maeneo hayo yamefungwa na shughuli mbalimbali zimesimama pamoja na Ofisi mbalimbali zimefungwa kutokana na hofu kubwa iliyotanda.
Kwa mujibu wa matangazo ya moja kwa moja ya Redio One wananchi wanakimbizana hovyo kukimbia mabomu ya machozi yaliyokuwa yakipigwa na Polisi kuwatawanya waumini waliokuwa wakitoka msikitini.
Hata hivyo taarifa kutoka eneo la tukio zinasema kuwa, waumini hao wameweza kutawanywa na hali bado tete huku magari ya jeshi la Polisi yakielekea katika maeneo ya Kinondoni ambapo kunadaiwa kuwa hali si shwari na vurugu kama hizo zinaendelea.
Na habari zilizotufikia sasa hivi Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limepeleka vikosi vyake katika maeneo ya Kariakoo ambapo vurugu zimekuwa kubwa ili kutuliza hali ya uvunjifu wa amani.

Muda si mrefu nilipishana na lori 3 za JWTZ pale Morocco zimejaa askari wakiwa na bunduki wakielekea mwelekeo wa Mwenge
Ujumbe wa simu kutoka kwa mtu wa karibu:
“Kuna taarifa kuwa Polisi wamelazimika kulipua mabomu katika maeneo ya Kariakoo na Chang'ombe ili kuwatawanya waandamanaji. Mimi kwa sasa nipo maeneo ya Mikocheni. Hapa nilipo hamna vurugu”

“Imagine
hiyo ni Posta Mpya sasa hivi (saa tisa alasiri) hakuna magari
yanayoingia” (picha na ujumbe kutoka kwa rafiki aliyepo eneo hilo)
Eneo la kati, jijini Dar es Salam (picha: Dkt. V. Mahamba)
No comments:
Post a Comment