George Nimayou ambaye siku za nyuma aliibuka na kudai marehemu Steven Kanumba alikuwa freemason, amefariki dunia ghafla.
Haruni Sanchawa na Makongoro Oging'
TAARIFA zilizotufikia wakati tunakwenda mtamboni zinadai kuwa, yule kijana aliyefahamika kwa jina la George Nimayou ambaye siku za nyuma aliibuka na kudai marehemu Steven Kanumba alikuwa freemason, amefariki dunia ghafla.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kilichoomba hifadhi ya jina, kijana huyo alifariki dunia Septemba 29, mwaka huu huko Tabata jijini Dar alikokuwa akiishi na kifo chake kinafananishwa na kile cha marehemu Kanumba.
Chanzo hicho kilidai kuwa, siku ya tukio zilisikika kelele ndani ya chumba alichokuwa akiishi na baada ya muda alitoka mwanamke na kutokomea kusikojulikana.
“Hatukujua kilichotokea, tulipoingia ndani tukakuta George amekufa ndipo taratibu za mazishi zilipofanyika,” kilidai chanzo hicho.
Wakizungumzia tukio hilo, baadhi ya watu wanaoishi eneo hilo walieleza kushangazwa na tukio hilo huku baadhi wakishindwa kuamini na kuhisi huenda alikuwa anarekodi filamu.
“Na sisi tunasikia tu kuwa eti kafariki lakini mbona msiba wenyewe hatukuusikia na hata picha za tukio zinaonesha watu wachache sana, sisi tunahisi kuna kitu nyuma ya tukio hili, hatuamini kuwa amekufa, “ alisema Mariam Hassan wa Tabata.
Ijumaa Wikienda lilizungumza na mmoja wa maofisa wa polisi Mkoa wa Ilala ambaye hakupenda jina liandikwe gazetini kwa kuwa si msemaji wa jeshi hilo ambapo alisema, hawajapata taarifa ya tukio hilo na kwamba huenda ni uzushi hivyo waandishi wetu wanaendelea kuifuatilia kwa kina, ikikamilika itaenda hewani.
No comments:
Post a Comment