MSANII wa Filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amefunguka kuwa heshima aliyonayo staa wa Muziki wa Bongo fleva, Joseph Lushalu `Bwana Misosi’ ndiyo iliyomfanya ampe penzi lake.
Akichonga na Tollywood Newz, Amanda alisema yeye siyo kama wanawake wengine ambao wanavutiwa na sauti,swaga na sura, bali amempenda Bwana Misosi kutokana na heshima aliyonayo katika jamii.
Joseph Lushalu `Bwana Misosi’.
“Bwana Misosi hana dharau, anawaheshimu wakubwa na wadogo pia ana mapenzi ya dhati tofauti na wanaume wengine wa siku hizi,” alisema.Aidha, alisema kuwa kutokana na hivyo anampenda mpenzi wake huyo kuliko kitu chochote na anamuomba Mungu ayaendeleze mapenzi yao ya dhati ili wadumu milele.
Habari Na Gladness Mallya
Habari Na Gladness Mallya
No comments:
Post a Comment