KAMA ulikosa kuhudhuria kwenye tamasha kubwa la Serengeti Fiesta 2012 ‘Bhaas!’ lililotimua vumbi kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam wikiendi iliyopita, mtumbuizaji mkuu akiwa ni Rick Ross ‘The Boss’ kutoka Kiwanja, basi ulikosa bonge la uhondo kutoka kwa wasanii damu changa wa Bongofleva ambao walionesha mapinduzi makubwa kwenye gemu, timu ya Over The Weekend inakujuza.
Ukiwafananisha na wakongwe kama MwanaFA, TID na wengine kibao, utagundua kuwa Fiesta ya mwaka huu imetawaliwa na wasanii wengi damu changa ambao ama kwa hakika wamedhihirisha kuwa wanakubalika kinomanoma kwa mashabiki wao, watazame Rich Mavoco, Stamina, Mabeste, Godzilla, Cyril, Nick wa Pili, Recho na wengine kibao walivyowachizisha mashabiki wao na kushangiliwa kwa nguvu. Ebwana Daaah!
“Hii ni kama taa nyekundu kwa wakongwe, wasipokaza buti huu ndiyo mwisho wao. Hawa wasanii chipukizi wana ‘njaa’ ile mbaya na wanajua wanachokifanya jukwaani, nawatabiria makubwa Rich Mavoco, Stamina, Nick wa Pili na wengine kibao. Wakongwe wanaonekana kuishiwa mbinu na wanapigia shoo uzoefu tu,” Zainab Abeid, mdau mkubwa wa burudani aliyekuwa analifuatilia tamasha hilo kwa umakini, aliiambia Over The Weekend.
No comments:
Post a Comment