KAMPUNI ya Tanzania Tooku Garments iliyoanza uzalishaji wa nguo za jinsi hapa nchini, imeahidi kuajiri Watanzania 2,000 ifikapo Julai, 2013.Ahadi ya ajira hizo ilitolewa katika taarifa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana ikieleza kuwa hadi sasa kampuni hiyo imeajiri wazawa 250 wanaozalisha nguo 35,000 kwa mwezi na kuongeza kuwa lengo ni kuzalisha nguo 300,000 kwa mwezi ifikapo Julai mwakani.
Malengo ya kampuni hiyo tanzu ya JD United Manufacturing inayomilikiwa na Wachina, ni kuajiri watu 500 wataozalisha jinsi 70,000 kwa mwezi hadi mwisho wa mwaka huu.
Kampuni hiyo inayoendesha shughuli zake chini ya Mpango wa maeneo maalum ya uzalishaji na mauzo nje (EPZ) ipo ndani ya ukanda wa kiuchumi wa Benjamin William Mkapa, eneo la Ubungo.Tanzania Tooku Garments ni miongoni mwa wawekezaji ambao EPZA imefanikiwa kuwashawishi kuja kuwekeza nchini kwa ajili ya kuongeza mauzo nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment