Rick Ross akifanya makamuzi ya hatari ndani ya Leaders Club.
Mwanamuziki mahiri kutoka nchini Marekani, William Leonard Roberts II 'Rick Ross' usiku wa kuamkia leo amehitimisha burudani za Serengeti Fiesta kwa mwaka huu baada ya kupiga shoo bab kubwa ndani ya Viwanja vya Leaders Club. Msanii huyo amewapagawisha mashabiki ambapo wengine wameshindwa kujizuia na kujikuta wakitaka kuvunja uzio ili angalau waamsogelee karibu kitendo kilichowapa kazi ya ziada mabaunsa waliokuwa katika viwanja hivyo.
(PICHA / HABARI : CLARENCE MULISA, MUSA MATEJA, RICHARD BUKOS NA ERICK EVARIST / GPL)
No comments:
Post a Comment