MWIGIZAJI
na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood, Simon Mwapagata ‘Kapturado’
amewashauri wasanii walioingia katika tasnia ya filamu wakitokea katika
tasnia ya ulimbwende warudi huko baada wao kuwa ni chanzo cha kashifa
katika tasnia ya filamu Bongo Rado anasema kuwa walimbende hao ndio
wanaovuma kwa matukio ngono na mavazi ya kujifedhehesha.
“Mimi
nikiwa kama mwanzilishi ya Bongo Movie Unity nina uchungu sana na tabia
ya hawa akina dada waliovamia tasnia ya filamu wakitokea katika fani ya
urembo wamekuja kutuharibia tasnia ya filamu kwa kufanya matukio ya
ajabu ajabu, ngono mara mavazi ya nusu uchi hiyo siyo filamu
ninawashauri warudi kwa Lundenga ndio anawezana nao,”anasema Rado kwa
uchungu.
Rado
amedai kuwa sababu kubwa ya kuanzishwa kwa kundi hilo ililenga
kubororesha tasnia ya filamu na si sehemu ya baadhi ya wasanii kuja
kujiuza au kuvaa nusu uchi katika majukwaa kama ambavyo imekuwa
ikifanyika madongo yaliwalenga wasanii ambao ambao ni gumzo kwa kashifa
Bongo Aunty Ezekiel na Wema Sepetu ambao wote waliingia katika tasnia ya
filamu wakitokea umiss.
Chanzo: habari hii ni kwa hisani ya www.filamucentral.co.tz
No comments:
Post a Comment