Stori: Haruni Sanchawa na George Kayala - Chanzo cha habari www.globalpublishers.info
VITA nzito imeyakumba makanisa ya kiroho nchini baada ya wachungaji wao hivi karibuni kurushiana maneno makali hadi wengine kutamka kuwa wenzao wanadanganya waumini ili kujipatia fedha.

Aliyeanzisha mtifuano huo
ni Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo, maarufu kwa
jina la Mzee wa Upako ambaye alikwenda mbali zaidi na kuwaonya waumini
wa Kikrito kujiepusha na watumishi wa Mungu wanaojiita mitume na
manabii, akidai kuwa wanafanya utapeli wa mchana.
Kwenye mahubiri yake kupitia kipindi kilichorushwa hewani na Televisheni za Channel 10 na C2C za jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mzee wa Upako, aliwaambia waumini kutoka makanisa ya Anglikana, Lutherani, SDA na Roman Katoliki waliojiunga na makanisa ya kiroho kuwa ni bora wakarudi katika makanisa yao ya awali kuliko kwenda katika makanisa ya wanaojiita mitume na manabii.

“Makanisa yetu haya ya kiroho ni hovyo, wameingia matapeli
na ninayasema hapa haya kwa kuwa ninayajua, nipo ndani ndiyo maana najua
kitu ninachokisema na mtu akitaka tubishane kwa hoja hii, hawezi
kunishinda.
“Najua hili ninalozungumza ni jambo zito na ni vita lakini ninaposema haya maneno ni sauti ya Mungu mwenyewe inatoka kupitia kinywa changu. Sitakuwa tayari kama mtumishi wa Mungu kuona watu wakiibiwa halafu nikaendelea kukaa kimya,” alisema Mzee wa Upako.

Aliongeza
kuwa ni bora aache kazi ya uchungaji anayoifanya, arudi kijijini kwao
akawe mkulima kuliko kukaa kimya akishuhudia watu wakiibiwa fedha zao na
watu wanaojiita mitume na manabii.
“Siyo siri, serikali inatambua Kanisa la Romani Katoliki, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Kanisa la Anglikana Tanzania, Kanisa la Mennonite na kidogo kwa sasa Kanisa la SDA.Makanisa yetu tunayoyaongoza ya kiroho nami nikiwamo, serikali haiyatambui na imetokana na watu kujiita mitume na manabii.
Baadhi ya watu wanaojiita mitume na manabi ni Josephat Mwingira wa Kanisa la Huduma ya Efatha, Onesmo Ndegi wa Living Water, Flora Peter wa Kanisa la Maombezi na Moses Kingu.
WALICHOSEMA WANAOJIITA MITUME
Gazeti hili liliwatafuta watu wanaojita mitume au manabii na walionesha kuna bifu kati yao na Mzee wa Upako kwani walikuwa na haya ya kusema:
Mtume Moses Kingu:

“Kila
mtu ana uhuru wa kusema, kauli aliyoitoa Mzee wa Upako huo ndiyo
mwisho wa fikra zake, pengine alisema hivyo kwa kulinda watu wake
wasimkimbie. Kauli yake hiyo ni ya kujiweka sawa, ukisoma Agano Jipya
unakutana na ufafanuzi wa mitume na manabii.”
Naye Nabii Onesmo Ndegi alisema: “Mzee wa Upako anatafuta umaarufu kwa kutumia kauli zake hizo kwani hata Biblia inatutambua. Angalia Wakorinto1, mlango wa 12 mstari wa 28 unaeleza kazi za manabii na mitume, anayesema mitume na manabii hawapo huyo ni mkorofi.

Kwa upande wa Nabii Flora alisema:
“Huduma ya maombezi ni ya Mungu na mtumishi wa Mungu wa kweli hapaswi
kumsema mtumishi mwenziye. Mtu wa namna hiyo kinachomsumbua ni wivu wa
waumini na utajiri na huwenda huduma yake imeanza kutetereka.
Nabii na Mtume Mwingira hakuweza kupatikana lakini katika kitabu chake alichokiita Wito Wangu na Kusudio Nililopewa, ameandika kuwa utume wake ni wa kupewa na Mungu.
Mwingira anasema alikuja kuchukuliwa duniani na malaika na akaenda mbinguni kwa kutumia ngazi.

Anaongeza
kuwa malaika aliyekuja kumchukua alimpeleka moja kwa moja kwa Yesu
ambaye alimkumbatia na akampeleka Jehanamu kuuona moto wa waovu.
No comments:
Post a Comment