MFANYABIASHARA maarufu mjini hapa, mwanamke mwenye asili ya
Kiasia, Previna Chade (60) amekutwa ameuawa nyumbani kwake na watu
wasiofahamika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ernest Magu alisema tukio hilo lilitokea Novemba 17, mwaka huu majira yasiyofahamika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ernest Magu alisema tukio hilo lilitokea Novemba 17, mwaka huu majira yasiyofahamika.
Mangu alisema siku ya pili baada ya kufanyika kwa
tukio hilo, majira ya mchana, majirani wa marehemu walipata wasiwasi na
kutoa taarifa polisi.
Alisema baada polisi kupata taarifa walikwenda hadi nyumbani kwa marehemu na kubomoa mlango, ndipo walipokuta amefariki dunia baada ya kupingwa na kitu kizito kichwani.
Alisema katika tukio hilo, polisi inawashikilia watu watatu kwa uchunguzi zaidi na mwili wa marehemu upo Hospitali ya Rufani Bugondo.
Wakati huohuo, watu watatu wamefariki dunia huku 24 wakijeruhiwa baada ya basi linalofanya safari zake kutoka Mwanza kwenda Magu kupata ajali baada ya kuacha njia na kupinduka.
Kamanda Mangu alisema ajali hiyo ilitokea saa 12:00 asubuhi katika Kijiji cha Isangijo, wilayani Magu kutokana na mwendokasi.
Alisema kutokana na mwendokasi, dereva alishindwa kudhibiti gari hilo, hali iliyosababisha kupoteza mwelekeo kwa kuacha njia na kuingia porini kisha kupinduka.
Alisema baada ya kusababisha ajali hiyo, dereva
alikimbia na hajafahamika alipo kwa sasa na kwamba polisi inamsaka ili
afikishwe mahakamani.
Kamanda Mangu alisema miili ya marehemu
imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufani Bugando, huku baadhi ya majeruhi
wakiendelea kupata matibabu.
No comments:
Post a Comment