Ripoti kutoka Kusini Magharibi
mwa Uchina, zinasema kuwa watoto watano wa barabarani wamepatikana
wamekufa kwenye debe kubwa la taka.
Polisi wanashuku kuwa watoto hao walifariki baada ya kukosa hewa safi, baada ya kuingia kwenye debe hiyo kukimbia baridi.
Habari hizo za watoto wa kiume watano, wadogo wenye umri wa kama miaka 10, zimeshutua na kuwashangaza raia wengi wa nchi hiyo.
Matopasi walikuta miili ya watoto hao kwenye deba la taka, katika mji wa Bijie, katika jimbo la Guizhou.Polisi wanajaribu kutafuta familia za watoto hao.Via BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment