EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, November 6, 2012

WEMA AMHARIBU DIAMOND.

 CHANZO CHA HABARI NA www.globalpublishers.info.
Na Luqman Maloto
MISS Tanzania 2006-07, Wema Isaac Sepetu kabla ya mwaka 2010, alishahusishwa kimapenzi na wanaume kadhaa, akiwemo Khaleed Mohamed ‘TID’, Hery Samir ‘Mr. Blu’, Jack Pemba, Jumanne Kihangala ‘Mr. Chuz’, Hartmann Mbilinyi, Jumbe Yusuf, marehem Steven Kanumba ‘The Great’ na wengineo.

Wema na Diamond wakati penzi lao motomoto.

Mtoto mduchu anayefanya Bongo Fleva, Nasib Abdu Juma ‘Diamond’, alianza kung’ara mwaka 2010 pale aliponyakua tuzo tatu za Kili Music Awards na baada ya hapo, alijihesabu kuwa staa, hivyo kula sahani moja na mastaa ambapo sasa matokeo yanaelekea kumfelisha kimuziki.
Jumamosi iliyopita, Diamond alifanya shoo kwenye Fainali za Miss Tanzania 2012-2013 na jinsi alivyoonesha uwezo mdogo siku hiyo, wadau walinena kwamba kijana ameanza kufeli kimuziki, ule uhodari wake wa kucheza na jukwaa umepotea.
Diamond akipondwa na kushushwa hadhi, nyuma yake kuna maneno kuwa chanzo cha uwezo wa dogo huyo kushuka ni mapenzi na mhusika mkuu ni Wema. Ipo wazi kwamba Diamond na Wema wameshindwa kuachana licha ya kutangaza kufanya hivyo mara nyingi.

HUU NDIYO MWANZO WA MWISHO WA DIAMOND?

Mwanzo wa mwisho ni msemo kutoka kwenye maneno ya Kiingereza, The beginning of the end. Hoja ni kwamba kiwango kidogo alichokionesha Diamond kwenye jukwaa la Miss Tanzania ni ashirio baya kuwa huenda ndiyo mwanzo wa mwisho wake kutamba kimuziki.
Kilichoonekana siku hiyo ni kwamba Diamond hana jipya na zaidi ameanza kuwa mzito jukwaani. Amekosa ubinifu wa kumfanya shabiki amuone wa tofauti. Amebaki yuleyule, hivyo biashara yake inaelekea ukingoni.
Kwa macho rahisi unaweza kutoa kauli kwamba Diamond amebweteka au amelewa sifa lakini ukweli ubaki kwenye mstari kwake kuwa penzi la Wema ni kilevi kikali kwake ambacho kwa kasi ya ajabu kinampotezea dira.
Diamond baada ya kulewa mapenzi ya Wema, sasa amegeuka sokomoko au pampula. Na kwa sababu ‘bwa mdogo’ huyo asili yake ni Kigoma, kule mlevi huitwa mboregwa, kwa hiyo binti wa Balozi Isaac Sepetu, amemfanya staa wa wimbo wa Mbagala awe mboregwa wa mapenzi.
Kama zamani alipokuwa anafanya shoo, watu walikuwa hawakai, wanacheza na kumiminika jukwaani kumtuza, siku hiyo aliimba wapi! Akateremka kuwafuata mashabiki walipo lakini hakuna aliyesimama wala kuonesha kusisimkwa na shoo yake.  Napigia mstari, this is the beginning of the Diamond’s end.
Hivi karibuni katika shoo ya Fiesta 2012, Diamond alishindwa kupokea shangwe zilizozoeleka, hata alipoamua kuvua nguo na kubakisha ile ya ndani, bado alichemka. Zaidi akaonekana kuharibu zaidi kuliko kujenga.
Diamond alivua nguo, kipindi ambacho Wema yupo kwenye gumzo zito kutokana na jinsi ambavyo alikuwa anacheza nusu uchi jukwaani katika shoo kadhaa za Fiesta 2012. Kwa maana hiyo, Diamond alipovua nguo ilitafsiriwa amemuiga Wema.
Unapomuiga mtu maana yake unakuwa umemkubali, kwa hiyo Diamond ‘amechizika’ kwa Wema kiasi ambacho hata uchafu anaoufanya yeye anauiga. Kwa mantiki hiyo Diamond na Wema ni kama boyfriend kama girlfriend (like a boyfriend like a girlfriend).

DIAMOND ANAHARIBIKA SI UTANI

Hapati muda wa kufanya mazoezi, anatumia muda mwingi kujiuguza maradhi ya mapenzi. Hii ndiyo sababu kwamba sikushangaa kumuona akichemka jukwaani. Wala sijiulizi ni kwa nini kiwango chake kinaporomoka kwa kasi.
Oktoba 26, 2012 usiku wa kati ya saa 8 na 9, nikiwa naendesha ‘kibebi-woka’ changu nikitokea ofisini kwetu Bamaga, Mwenge, naelekea nyumbani Kijitonyama, nilipofika Mtaa wa Akachube (Kijitonyama), nilimkuta Wema akiwa anaongea na simu huku amezungukwa na watu.
Nikafunga breki, nikashusha kioo nikamsalimia naye akaitika. Nilipoona hayupo kwenye hali ya kawaida nikashuka. Stori niliyoipata pale ni kuwa kumbe alikuwa amegombana na Diamond muda mfupi uliopita.
Eneo la tukio (jirani kabisa na kwa Wema), alikuwepo pia mwanamuziki Omar Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’. Nilipoona mazingira hayavutii, nikamuacha Ommy anamtuliza Wema, mimi nikaondoka zangu.
Asubuhi nikaambiwa kuwa Diamond alirudi nyumbani kwa Wema, suluhu ikapatikana. Jaribu kufikiri kuwa kama mtu usiku wa manane yupo bize na mapenzi, migogoro isiyokwisha ni saa ngapi atatulia kubuni shoo? Ni muda gani atautenga kwa ajili ya kutengeneza staili mpya?

JE, ANAYAJUA YALIYOMKUTA KANUMBA KWA WEMA?

Mungu amlaze mahali pema marehemu Kanumba ambaye ndiye aliyemfanya Wema aingie kwenye ulimwengu wa filamu. Mapenzi yalipokolea, The Great alilewa kiasi kwamba alishindwa kabisa kustahimili vishindo.
Kwa mara ya kwanza Kanumba aliripotiwa kupigana kwa sababu ya Wema. Staa huyo wa filamu akawa hatulii, mara yupo polisi kwa sababu ya kesi ya Wema, ufanisi wake ukaporomoka. Nadhani kuna kitu, sasa namuona Diamond anashika mkondo uleule.
Kanumba aliposhtuka alimuacha Wema na kuanzia hapo alirudi kung’ara kwenye soko la filamu. 
Wema alimchonganisha Kanumba na Jumbe wakapigana, mwanamke huyo kawachonganisha Diamond na hasimu wake, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior’. Ikidaiwa kuwa mrembo huyo amempa penzi Bob Junior.

Itaendelea wiki ijayo.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate