EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, December 10, 2012

JACK WOLPER AMTAMBULISHA RASIMI MCHUMBA WAKE KWA MBWEMBWEE ZA MILIONI 19.

ALHAMISI iliyopita (Desemba 6, 2012), ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya Jacqueline Wolper, jioni yake ndani ya Synergy Lounge, Oysterbay, Dar es Salaam, alifanya bonge la pati, akiwaalika ndugu, jamaa, marafiki na majirani.

Mbele ya kila aliyehudhuria, Wolper alimtambulisha mchumba wake mpya ambaye amempiga bao, Abdallah  mtoro, ‘Dallas’ lakini akawaacha waalikwa na maswali lukuki pale alipogoma kumtaja jina.

Hakuishia hapo, akaomba mchumba wake huyo asipigwe picha hata ya kwenye simu, akisisitiza kuwa wana maana kubwa kuzuia hilo. 
Mara nyingi mwenye fedha hata kama hasemi, vitendo vyake huongea, na kelele za jamaa huyo zilisomeka kwa herufi kubwa pale ulipowadia muda wa kumtuza ‘mtoto aliyezaliwa’ ambapo alimtuza cheni zenye thamani kubwa.
Wale waliomwakilisha jamaa huyo, hawakusema bei iliyonunuliwa, badala yake mmoja wao alitamka: “Cheni hizi zina thamani kubwa, kuliko zawadi yoyote ambayo inaweza kutolewa hapa.”

Cheni hizo ni mbili, moja ya shingoni na nyingine mkononi.


Mastaa kibao walihudhuria sherehe hiyo, kila mmoja alishangweka vya kutosha, huku misosi ikiwa siyo ya kuuliza, keki ilikatwa na kuliwa, shampeni zilifunguliwa na matukio mengine mengi ya kuvutia.

MC wa shughuli hiyo, Salum Mchoma ‘Chiki’, aliichangamsha sherehe na uwepo wa staa wa vichekesho, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, ulisababisha mbavu za waalikwa ziteseke.

Wolper, alipomtangaza mchumba wake huyo, alizungumza kwa kujiamini na madaha ndani yake na kusababisha wegeni wengi washangilie, huku wachache wakipigwa na butwaa.

Mmoja wa mastaa waliopigwa na butwaa, alihojiwa na ripota wetu na akajibu: “Kiukweli nilishangaa, unajua maneno yaliyokuwepo ni kwamba baada ya kuachana na Dallas angefulia lakini leo imekuwa tofauti ndiyo maana nimeshtuka kidogo.”

Staa huyo , alipoona atatafsiriwa vibaya, akaongeza kama aliyekumbuka kitu: “Lakini naomba ieleweke mshtuko wangu ni wa heri. Nampenda Wolper na namtakia maisha mema na huyo mchumba wake.”


Wapambe waliokuwa na mchumba huyo wa Wolper, walizungumza kwa kishindo ukumbini: “Kama kuna mtu alikuwa na mategemeo kwamba huyu mrembo atapata shida, hayo mawazo aondoe kabisa.

“Tunajua kila kitu kwamba Wolper alikuwa na mtu ambaye alishindwa kumgharamia, kwa hiyo hapa kafika. Tutamhudumia vizuri sana.”

 Kwa mjibu wa Wolper, sherehe hiyo imegharimu shilingi 19,600,000.

“Nawashukuru sana marafiki zangu waliokuja kunisapoti kwenye sherehe hii maana nimejisikia faraja ambayo sikutegemea kuipata kwa leo.

“Nimetumia milioni 19 na laki 6 kwa ajili ya kuandaa sherehe hii ili niwaburudishe marafiki  na ndugu zangu, ingawa kwa haraka haraka wengi ukiwatajia fedha hii wataona ni nyingi ila waliyokuwemo ukumbini wenyewe wataamini maana vinywaji na vyakula vyote vilikuwa vikitoka humo humo na hatukununua nje.”
                         Chanzo cha habari ni Grobal Publishers.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate