LEO
katika mji wa Morogoro burudani ni moja tu, Jahazi Modern Taarab,
wakazi wote wa mji huu wanaongea lugha moja leo, JAHAZI, hakuna kitu
kingine zaidi ya Jahazi.
Ni onyesho maalum la mkesha wa X-Mas sambamba na utambulisho wa nyimbo mpya zilizomo ndani ya albam mpya ya “Wasiwasi wako”.
Tayari
kundi zima la Jahazi chini ya Mzee Yussuf limeshawasili Morogoro tangu
saa 8 mchana, kilichobakia ni wasaa tu wa kwenda kwenye ukumbi wa Savoy
kuwapa raha wakazi wa mji huu ambao huwa huwaambii kitu kwa Jahazi.
Onyesho linatarajiwa kuanza saa 3 usiku hadi 9 za usiku.
No comments:
Post a Comment