Mwandishi
wa habari wa Kampuni ya Free Media inayochapisha magazeti ya Tanzania
Daima na Sayari, Shaaban Matutu akionesha jeraha lililotokana na kupigwa
risasi na Polisi katika tukio lililotokea usiku wa kuamkia leo - baada
ya polisi kuvamia nyumbani kwake Tegeta jijini Dar es Salaam kwa madai
ya kumtafuta mtuhumiwa waliyekuwa wakimsaka. Matutu kwa sasa amelazwa
Hospitali ya Muhimbili katika Kitengo cha Mifupa (MOI) kwa ajili ya
matibabu zaidi.
Shabaan
Matutu akionesha sehemu ya mkono wake wa kulia ambao ulipata majeraha
wakati polisi walipotumia nguvu kuingia chumbani kwake na kumtwanga
risasi iliyompiga upange wa kushoto wa kifua chake.
Daktari
aliyekuwa zamu katika Hospitali ya Mwananyamala akiangali picha ya
X-Ray ya Matutu mara baada ya kufikishwa katika hospitali hiyo na
kufanyiwa kipimo hicho, kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Wafanyakazi
wa Free Media, Khadija Kalili (kushoto) na Maria Kayala (kulia) ambao
walifika Hospitali ya Mwananyamala baada ya kupata taarifa za tukio hilo
wakiwa na Matutu.
(Picha / Habari na Dande Francis)
No comments:
Post a Comment