PICHA ambayo staa wa filamu Bongo, Tamrina Mohammed Poshi ‘Amanda’
aliyoipiga na marehemu Hussein Mkieti ‘Sharo Milionea’ inamkosesha
usingizi kila akiitazama.
Tamrina Mohammed Poshi ‘Amanda’ akiwa na marehemu Hussein Mkieti ‘Sharo Milionea’.
Akizungumza Risasi hivi karibuni, Amanda alisema picha hiyo waliipiga
wakati wa mwezi wa Ramadhani (Septemba, mwaka huu) ambapo Sharo
Milionea alifunguka kuwa anatamani kufanya naye kazi, kweli wakafanya
naye kazi ya pamoja katika mazingira ambayo hawezi kuyasahau.
“Mazingira ya yale mazungumzo yetu yanaponijia huwa nakosa usingizi kabisa. Tulifanya naye filamu ya Kitu Bomba ambayo haijatoka mpaka sasa lakini kwa kweli sasa hivi ananipa wakati mgumu sana, Mungu amlaze mahali pema peponi,” alisema Amanda.

No comments:
Post a Comment