IDADI
ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Ukimwi katika Wilaya na Mkoa wa
Geita, inasemekana imeongezeka katika kipindi cha mwaka 2011/12 kufuatia
hatua ya baadhi ya wagonjwa, kuacha kutumia dawa za kupunguza makali ya
virusi baada ya kwenda Loliondo kwa babu na kupata kikombe cha dawa.
Hali
kadhalika kuwapo kwa shughuli za migodi ya wachimbaji wadogo na uvuvi
katika Ziwa Victoria, kumechangia ongezeko la vifo vya watu kutokana na
ugonjwa huo.
Imeelezwa kuwa ongezeko la shughuli za kiuchumi katika maeneo ya madini na uvuvi, ni changamoto kubwa kwa idara ya afya wilayani humo katika kupambana na kasi ya maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi kwa wakazi wa Geita.
Imeelezwa kuwa ongezeko la shughuli za kiuchumi katika maeneo ya madini na uvuvi, ni changamoto kubwa kwa idara ya afya wilayani humo katika kupambana na kasi ya maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi kwa wakazi wa Geita.
Mratibu
wa Mpango wa Kudhibiti Ukimwi katika Wilaya ya Geita, Patrisia Masinde,
aliiambia Mwananchi jana kuwa katika kipindi cha kati ya Januari na
Novemba mwaka huu, watu 31 walipoteza maisha kutokana na ugonjwa huo
ambao hadi sasa haujapata tiba. Alisema watu hao ni sehemu ya watu
131,waliokuwa wamelazwa katika vituo vya afya wakipata huduma.
Masinde
alisema idadi ya vifo vilivyotokana na Ukimwi katika wilaya hiyo katika
kipindi hicho, vimeongezeka kwa asilimia mbili ikilinganishwa na
kipindi kama hicho mwaka jana.
Kwa mujibu wa mratibu huyo, katika kipindi hicho mwaka jana, watu waliopoteza maisha kwa ugonjwa huo walikuwa 16.
Kwa
upande wake, Mratibu wa Ukimwi katika Kitengo cha Matibabu katika
Wilaya ya Geita, Dk.John Mgosha alisema vifo hivyo vinatokana na baadhi
ya wagonjwa waliokwenda kwa Babu wa Loliondo na kupata kikombe cha dawa,
kuacha kutumia vidonge vya kuvumbaza virusi vya Ukimwi.
Alisema
baadhi ya watu hao Loliondo waliamini kwamba Mchungaji Amilikile
Masapila, alikuwa na dawa ya kutibu ugonjwa wa Ukimwi licha ya kutambua
kuwa hakuna dawa iliyothibitishwa na watalaamu wa afya kutibu ugonjwa
huo.
Chanzo: www.mwananchi.co.tz
No comments:
Post a Comment