Mwanamitindo
wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata ambaye ameng’ara kimataifa
baaada ya kushinda tuzo ya Nigeria’s Next Super Model na kuwa
mwanamitindo bora barani Afrika wa mwaka 2012 (Africa’s Most Outstanding
Model 2012).
Flaviana katika pozi.
---
MWANAMITINDO wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata ameendelea
kung’ara kimataifa baaada ya kushinda tuzo ya Nigeria’s Next Super Model
na kuwa mwanamitindo bora barani Afrika wa mwaka 2012 (Africa’s Most
Outstanding Model 2012).
Tuzo hiyo utolewa kwa wanamitindo ambao bado wanailetea sifa Afrika
kimataifa na Flaviana amekuwa katika chati ya juu. Mwaka jana Desemba,
Flaviana alishinda tuzo nyingine ya uwanamintindo bora kutoka kwa
diaspora ya Waafrika.
Flaviana ambaye kwa sasa anaishi na kufanya kazi ya uanamitindo
New York nchini Marekani kupitia shirika la Wilhelmina Models, mpaka
sasa ameweza kuitangaza Tanzania kimataifa kutokana na umahiri wake
katika maonyesho ya mavazi.
Tangu ashinde taji la Miss Universe Tanzania mwaka 2007, Flaviana
amekuwa aking’ara katika kona zote za dunia na hasa baada ya kumaliza
katika nafasi ya sita katika mashindano ya kimataifa ya Miss Universe,
huku Tanzania ikishiriki kwa mara ya kwanza.
Ameweza kushiriki katika maonyesho ya mavazi mengi Ulaya na Amerika
huku akitoa misaada mingi kwa Watanzania wenzake ambao wamekuwa na
ndoto ya kufika mbali katika fani hiyo.
Kwa sasa Flaviana anaendesha taasisi yake, Flaviana Matata
Foundation ambayo inasomesha watoto wa kike 16 na mwaka jana alitoa
msaada wa vifaa vya kuokoa maisha kama sehemu ya kumbukumbu ya kuzama
kwa meli ya MV Bukoba huku ikiwa kumbukumbu ya kifo cha mama yake mzazi
katika ajali hiyo ya mwaka 1996.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Compass Communication Tanzania
Limited, Maria Sarungi Tsehai alisema kuwa wamejisikia faraja sana kwa
kumvumbua mwanamitindo huyo ambaye kwa sasa anashika chati ya juu
Tanzania na nje ya nchi.
Maria alisema kuwa Flaviana amedhihirisha ubora wake na mpaka sasa
amepitiliza kiwango cha kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake, ndoto
ambayo alikuwa nayo muda mrefu.
HABARI NA FULL SHANGWE BLOG
No comments:
Post a Comment