UONGOZI wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo
cha Usimamazi wa Fedha (IFMSO) cha jijini Dar es Salaam, umesema hali ya
usalama kwa sasa katika Hosteli za Kigamboni inaridhisha.
Waziri Mkuu wa IFMSO, Daniel Sarungi alisema jana
kuwa tangu iundwe timu ya polisi inayoshirikiana na wanafunzi hao hali
imekuwa tulivu kwa kipindi cha wiki moja iliyopita.
Sarungi alisema kuwa hakujatokea uvamizi tena katika hosteli zao, lakini akaongeza kusema kuwa taarifa kamili ya ripoti ya timu hiyo itatolewa na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova.
Sarungi alisema kuwa hakujatokea uvamizi tena katika hosteli zao, lakini akaongeza kusema kuwa taarifa kamili ya ripoti ya timu hiyo itatolewa na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova.
“Kuna amani sana, misako imefanyika lakini ripoti itatolewa Januari 30 na Kamanda Kova,” alisema Sarungi.
Kauli ya Kiongozi huyo wa wanafunzi haikutofautina na ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke, Englbert Kiondo, ambaye alisema taarifa inayohusu hali ilivyo itatolewa na Kamanda Kova.
Kwa upande wa wakazi wa Kigamboni, walisema kuwa wameshuhudia polisi wakifanya doria maeneo hayo tofauti na ilivyokuwa huko nyuma kabla wanafunzi hawajaandamana.
Walisema pia wameona polisi wakiwakamata wahalifu
kwenye maeneo hayo kutokana na misako wanayoifanya hali ambayo imeleta
utulivu kwenye mji huo.
“Kwa sasa kumetulia inawezekana wanasikilizia
(wahalifu), likini ingetakiwa polisi wawakamate wale vinara kwa sababu
wanawafahamu” alisema Salum Rashid mkazi wa eneo hilo.
Naye mkazi mwingine anayejishughulisha na biashara
ya kioski, alisema kuwa kumekuwa na utulivu kwani hata wanafunzi ambao
ndiyo wateja wake wakubwa wanamwambia kuwa wanaweza kuacha vitu
wakavikuta salama.
Eneo la Kigamboni lilikuwa tete wiki iliyopita
ambapo wanafunzi hao waliandamana kupinga vitendo vya udhalilishwaji
walivyokuwa wakifanyiwa na wahalifu.
Wakati huohuo, Mwandishi Wetu Peter Edson
anaripoti kuwa, Meya wa Manispaa ya Ilala,
Jerry Silaa amesema ili kufanikisha mapambano dhidi ya uchafunzi wa mazingira jijini Dar es Salaam elimu ya usafi mabadiliko kifikra na kimtazamo vinatakiwa kwenda sambamba.
Jerry Silaa amesema ili kufanikisha mapambano dhidi ya uchafunzi wa mazingira jijini Dar es Salaam elimu ya usafi mabadiliko kifikra na kimtazamo vinatakiwa kwenda sambamba.
Akizindua kampeni ya usafi wa mazingira jijini Dar
es Salaam Silaa alisema suala la usafi wa mazingira ni mtambuka hivyo
ni lazima elimu ianze kutolewa mashuleni hadi vyuoni ili watu waweze
kubadili fikra na mitazamo ya kudhani kuwa usafi unawahusu baadhi ya
watu tu.
Alisema jiji likiwa safi magonjwa ya milipuko
hayataweza kutokea lakini hivi sasa Mkoa wa Dar es Salaam umekuwa
ukikumbwa sana na magonjwa ya mlipuko kwa sababu ya uchafunzi wa
mazingira ulikithiri.
Naye meneja wa kampeni hiyo Elizabeth Stcheers alisema kwa sasa kampeni hiyo itahusisha kata tatu zilizopo katika Manispaa ya Ilala ambazo ni Kata ya kivukoni, Mchafukoge, na Kata ya Kisutu
Alisema huu ni mwanzo wa mpango ambapo baadaye zitahusishwa manispaa zingine katika Mkoa wa Dar es Salam lengo likiwa ni kuweka jiji safi na salama.
No comments:
Post a Comment