MCHEZA
filamu nyota wa kibongo, Rose Ndauka, anatarajiwa kupiga hatua nyingine
katika sanaa yake pale atakapoanza kuonekana kwenye luninga yako akiwa
na kipindi bab kubwa cha majadiliano (Talk Show).
Rose
Ndauka ameiambia Saluti5 kuwa kipindi hicho kitajulikana kama The
Family Talk Show na kinaandaliwa na kampuni ya Kikoi Tanzania Limited.
Hii
inakuwa ni hatua kubwa kwa Rose Ndauka na sasa atawekwa kwenye mizani
moja na vipindi kama Ongea na Janet na The Mboni Show ambavyo kwa sasa
vinakimbiza ile mbaya.
Rose Ndauka amesema The Family Talk Show kitakuwa hewani kati ya mwezi Februari na mwezi Machi huku kikiwa na mada za kusisimua.
Hata
hivyo Rose alipoulizwa kipindi hicho kitarushwa kituo kipi, alisema
hilo bado liko chini ya zulia. “Tutaeleza muda mfupia baadae juu ya
siku, muda na kituo gani” alisema Rose Ndauka.
Aidha
Rose Ndauka ameiambia Saluti5 kuwa ujiowa kipindi hicho haumaanishi
kuwa ndio mwisho way eye kucheza filamu. “Filamu ndio kazi yangu na
maisha yangu, nitaendelea kuigiza” alisema.
Via - Saluti 5
No comments:
Post a Comment