WAKATI fulani huwa najiuliza kwa nini tunakuwa na wapenzi, kwa nini
mapenzi yakawepo? Kwa nini tunaoa ama kuolewa? Kwa nini baadhi ya watu
huamua kujinyonga baada ya kuachwa na wapenzi wao?
Kwa nini mapenzi
yameharibu baadhi ya maisha ya watu? Huwa najiuliza maswali mengi yenye
kwa nini, yakihusisha mapenzi. Kwa ujumla kama nilivyo na maswali mengi,
majibu pia yamekuwa mengi.
Kwa
vyovyote itakavyokuwa mapenzi ni sehemu ya maisha yetu na kwa hakika
maisha hayawezi kukamilika bila mapenzi. Ninapozungumza mapenzi
namaanisha yale yanayotoka moyoni mwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Mapenzi hayo, hukamilika baada ya wawili hao kuwa na hisia sawa za mapenzi. Amini kama upo katika uhusiano na mpenzi ambaye hakupendi, yaani wewe peke yako ndiyo uliyemzimikia, hatari kubwa iko mbele yako.
Nasema hatari iko mbele yako najua huwezi kuwa na mwisho mzuri. Kama ni msichana utachezewa na mwisho wa siku utaachwa solemba kwa kuwa tu uliyemruhusu aingie kwenye moyo wako hajakupenda kwa dhati.

Lakini
pia kukubali kuingia kwenye uhusiano na mtu ambaye moyo wako unasema
‘no’ siku za baadaye unaweza kujikuta unachukua maamuzi ambayo yanaweza
kuyaathiri maisha yako kwa kiwango kikubwa.
Kumbuka mapenzi ni nguzo ya maisha yetu tena nguzo muhimu sana. Kama ukifanikiwa kumpata mpenzi ambaye atakupenda na wewe ukampenda ni wazi kuwa maisha yako yatakuwa yenye furaha na hakika utatawaliwa na amani siku zote.
Wakati mwingine unaweza ukapendwa na mpenzi ambaye hujampenda. Yaani yeye anaonesha kukuzimikia ile mbaya huku akikuahidi mambo mazuri lakini ukijaribu kufanya mawasiliano na moyo wako unakujibu kuwa hauko tayari kumpokea.

Ukweli wa mambo ni kwamba, mtu huyo unatakiwa kumweleza
ukweli, yaani umkatalie kiroho safi tu kwa kuwa hakuna sababu za msingi
za kukufanya wewe ulazimishe kuwa naye. Unalazimisha kumpenda kwa sababu
za utajiri wake? Utakuwa unaidhulumu nafsi yako hivyo kwa kuwa moyo
wako umeshazungumza na wewe, umekuweka wazi kuwa hauna mapenzi ya dhati
kwa mtu huyo, muache apite.
Muache aende kwa kuwa, penzi linaloweza kukupa amani ni lile ambalo moyo wako umeridhia. Kulazimisha penzi eti kwa kuwa umeona jamaa ana fedha za kutosha ni sawa na kujiingiza kwenye kaburi wakati bado hujafa.
Uchunguzi wangu mdogo umenionesha kuwa, kuna wasichana wengi ambao maisha yao yako gizani kwa kuwa wamekubali kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na wanaume ambao hawawapendi.

Baadhi
wakitongozwa na mwanaume ambaye anaona wazi kuwa hampendi, lakini akawa
na mali au uwezo mkubwa kifedha, huamua kumkubali kwa lengo la kupata
vitu vya mwanaume huyo.
Hufanya hivyo akijidanganya kuwa eti atakuwa akiunda penzi taratibu kitu ambacho hakiwezi kufanyika na kama kitafanyika lazima usanii utakuwepo ndani yake.

Hili ni tatizo kubwa
na ndiyo maana nikaona leo nilizungumzie ili kuwanusuru wale
wanaohatarisha maisha yao kwa kukubali kuingia kwenye uhusiano/ndoa na
watu ambao hawawapendi kwa sababu ya tamaa zao.
Kuanzi leo, kama uko kwenye uhusiano hakikisha uliyenaye unampenda na si kwamba unalazimisha kumpenda kwa sababu ya mali alizonazo. Kama hujaingia kwenye uhusiano, kuwa makini na watu wanaokutokea, unayemkubali kuwa wako hakikisha moyo wako umemuidhinisha na si vinginevyo.

VIA MAHABA NA GLOBALPUBLISHERS
No comments:
Post a Comment