MTANDAO wa wanawake mkoani Kilimanjaro, umetaka Katiba Mpya
iweke usawa katika nafasi tatu za juu za uongozi; Rais, makamu wake na
Waziri mkuu ili mojawapo apewe mwanamke.
Licha ya nafasi moja kwa mwanamke, mtandao huo umependekeza katiba iwe katika misingi ya haki, utu, usawa na heshima na kupinga mila na desturi zinazomkandamiza na kumnyima haki mwanamke.
Alisema Tanzania imeridhia mikataba na matamko mbalimbali yanayokataza ubaguzi wa aina yoyote, alitolea mfano Sheria ya Ardhi ya Mwaka 1999 na Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 inatoa haki kwa mwanamke kumiliki, lakini sheria ya mirathi inanyang’anya haki hizo.
Pia, mtandao huo unataka katiba iainishe ushiriki wa wanaume katika afya ya uzazi, ikiwamo kukataza watendaji wabovu kuhamishiwa maeneo ya kazi pindi wanapokosea, badala yake washtakiwe.
Akitoa mada kwenye mkutano huo, Agnatha Rutazaa alisema sekta ya ajira kuna upendeleo mkubwa, kwani kipaumbele kinatolewa kwa wanaume zaidi hata kama mwanamke ana sifa sawa na mwanaume.
Alisema katiba inazungumzia jinsia, lakini kwenye uhalisia hakuna usawa na kutaka Katiba Mpya iweke usawa kati ya mwanamke na mwanaume.
No comments:
Post a Comment