Malkia wa Nyuki, Rahma Al Kharoos akizungumza jana |
Na Mahmoud Zubeiry
MFADHILI wa Simba SC, Rahma Al Kharoos amesema kwamba timu hiyo kwa sasa haistahili kufundishwa na kocha kutoka nje, kwa sababu haina wachezaji wataalamu na wenye ubora na viwango, hivyo amependekeza iwe chini ya mzalendo Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ pekee.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari jana katika hoteli ya Movenpick, Dar es Salaam,
Rahma maarufu kama Malkia wa Nyuki, amesema kwamba kama Simba wanataka
kuwa na makocha wa kigeni, basi watafute wachezaji wataalamu na wenye
ubora na viwango.
“Unajua
ukikaa ukiangalia timu inavyoendelea ya Simba, tofauti na uwezo wake na
kocha kutoka nje, sawa sawa na mtoto wa shule ya vidudu, unampa mwalimu
wa chuo kikuu. Kwani sisi hatuna makocha hapa, si tuna
makocha,”alisema.
Aidha,
Mama Salma ambaye jana aliahidi kumlipa malimbikizo yake ya mishahara
ya miezi mitatu kocha aliyetupiwa virago Simba SC, Mseriba Profesa
Milovan Cirkovick (dola za kimarekani 24,000), alisikitikia makocha wa
kigeni kupewa fedha nyingi, wakati wazawa wapo na wana uwezo.
“Fedha
hizi dola 8,000 (kwa mwezi) anayopewa (Milovan), makocha wangapi
watafaidika hapa, sasa hivi hii fedha inakweenda nje, faida yake nini,
kwa nini wasipewe makocha wazawa, wampe hiyo timu Julio,”alisema.
Mama alisema kwamba hakuna tatizo timu za Tanzania kufundishwa na makocha wazawa, kwa sababu nchi nyingi zinatumia makocha wazawa na akatolea mfano Oman kwamba timu nyingi zinatumia makocha wa Tanzania.

“Kwa
nini sisi tutafute makocha wa nje halafu hatuwezi kuwalipa, kwa sababu
gani, kwa sababu ya sifa, haiko hivyo, sasa hivi lazima tubadilike.
Mkwasa (Charles Boniface) alikuwa anafundisha Twiga Stars, timu ya
wanawake, timu ngumu zaidi, lakini ameifundisha na kaifikisha hapo
ilipo.
Huyo Julio si alikuwa Oman, si alikuwa anafundisha timu nzuri Oman, sasa tatizo liko wapi, tatizo tuwape fursa wenzetu hapa, kama mnataka kuleta makocha wa nje, tafuteni na wachezaji wataalamu, ambao watakuwa wapo kwenye ubora na viwango,”alisema Malkia wa Nyuki.

Kwa
sasa, Simba SC inafundishwa na Kocha Mfaransa, Patrick Liewig
anayesaidiwa na Mganda, Moses Basena na mzalendo Jamhuri ‘Julio’
asante:bin zubery wa www.bongostaz.com
No comments:
Post a Comment