KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, mwalimu mstaafu na mwanamke
mmoja ambaye ni muuguzi juzi walifumaniwa wakifanya mapenzi katika moja
ya vyoo vya Qman Grosary iliyopo mjini Geita.
Mwalimu huyo mstaafu ambaye amewahi kufundisha katika Shule ya Msingi
Nyamalembo, Kata ya Mtakuja na mwanamke huyo ambaye ni muuguzi katika
Hospitali ya Wilaya ya Geita (majina yanahifadhiwa) walifumaniwa baada
ya kutiliwa shaka na baadhi ya wananchi waliokuwa wakipata vinywaji
katika grosary hiyo.
Mmoja wa wafanyakazi wa grosary hiyo ambaye hakutaka jina lake
liandikwe alidai kuwa wawili hao walifika eneo hilo majira ya
mchana kwa lengo la kupata kinywaji.
Alisema kabla ya wawili hao kufanya uzinzi huo, walianza kufanya
vitendo vya aibu ikiwa ni pamoja na kunyonyana ndimi, jambo
lililowachefua baadhi ya wanywaji, hatua iliyomfanya awasihi kuondoka na
kutafuta sehemu ya kupumzika.
“Nilipowaona wamezidisha kufanya ufedhuli huo niliwasihi watafute
sehemu ya kupumzika kufanya mambo yao na si hadharani kama wanavyofanya,
lakini juhudi zangu hazikuzaa matunda, kwa kuwa hawakukoma,” alisema
mfanyakazi huyo.
Badala yake, aliwaona wawili hao wakiongozana kuelekea chooni mithili
ya watu wanaokwenda kujisaidia lakini walikawia kurudi na baada ya
kufuatilia aligundua kuwa walikuwa wakifanya mapenzi kwenye choo.
Mwalimu huyo alipohojiwa na mwandishi wa habari hizi alijitetea akidai
kuwa hakujua akitendacho na kwamba ilikuwa ni kwa sababu ya kulewa mno.
Hata hivyo, alimtishia mwandishi wa habari hizi akimwonya kutoandika tukio hili akidai vinginevyo angemdhuru.
“Hiyo ilikuwa pombe na wala mimi si wa kwanza kufanya hivyo, hivyo
iwapo unataka kuishi katika umri ambao Mungu amekupangia nakuomba
uachane na habari hiyo, mimi ni komando na ikitoka uombe niamke
nimekufa,” alisema mwalimu huyo.
Naye muuguzi huyo alijitetea kuwa alilazimishwa kufanya kitendo hicho
na mwalimu huyo baada ya kumdanganya amsindikize chooni na walipofika
alifunga mlango na kisha kumvua nguo na kumuingilia kwa nguvu, akidai
aliogopa kutoa taarifa polisi kuhofia ndoa yake kuvunjika.
No comments:
Post a Comment