EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, February 12, 2013

Spika Anne Makinda apokea jumbe 600+ zenye wito wa kujiuzulu na matusi

Inatipotiwa kuwa Spika wa Bunge, Anne Makinda, amepokea jumbe za maneno 400 na za miito ya simu 200 zenye matusi ya nguoni kutoka kwa watu wakimtaka ajiuzulu. Mtoa h abari wa HabariLeo ambaye yupo karibu na Spika Makinda amesemea jumbe hizo zimerekodiwa.

Kwamba, Spika alianza kupokea jumbe hizo kuanzia juzi, baada ya viongozi wa CHADEMA kutangaza namba za simu za Spika kwenye mkutano wa hadhara na kuendelea jana ili kutumia ‘nguvu ya umma’, kumlazimisha ajiuzulu.

Sababu ya kutumwa jumbe hizo inaripotiwa kuwa ni baada ya hatua ya Spika Makinda kutangaza mabadiliko ya Kamati za Bunge, yaliyoivunja Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na shughuli zake kuwekwa chini ya Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) ambapo katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Mwenyekiti wa POAC, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe hakuridhishwa nayo na hivyo kumshitaki Spika Makinda kwa Wananchi ili wamng’oe.

Unaweza kutizama/sikiliza wito huo kupitia audio na video ya chapisho/post ya awali (bofya hapa).
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah, alipozungumza na gazeti hili juzi, alisema uamuzi huo haukufanywa na Spika Makinda peke yake, bali ni baada ya kushauriana na Kamati ya Kanuni za Bunge, ambayo iliridhika na sababu za kuchukuliwa uamuzi huo.

Wajumbe wa Kamati iliyoridhia makubaliano hayo mbali na Spika na Naibu Spika, ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA). Wengine ni Mbunge wa Mbulu, Mustapha Akunaay (CHADEMA), Mbunge wa Kibondo, Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi), Mbunge wa Mkanyageni, Mohamed Habib Mnyaa (CUF) na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF). Pia Mbunge wa Viti Maalumu, Anna Abdallah (CCM), Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM), Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ramo Makani (CCM), Mbunge wa Viti Maalumu, Pindi Chana (CCM) na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono (CCM).

Dk Kashilillah alisema mabadiliko hayo hayakuigusa kamati ya POAC peke yake, bali kamati zingine kama ya Sheria Ndogo na ya Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje, ambayo imegawanywa mara mbili.

Akielezea sababu za kuvunja POAC, Dk Kashilillah alisema lengo lilikuwa ni kuunganisha wizara, taasisi zake na mashirika yaliyo chini ya wizara husika, ili yawe na msemaji mmoja.

Alisema awali Waziri alikuwa anawajibika PAC, wakati mashirika ya umma yaliyo chini ya wizara yakiwajibika chini ya POAC.

Kwa mujibu wa Dk Kashilillah, kulikuwa na mkanganyiko mkubwa na akaeleza kuwa hatua ya kuunganisha wizara na mashirika yake ya umma, kutafanya sasa Waziri, Katibu Mkuu, Mwenyekiti wa Bodi na watendaji wakuu wa mashirika, kuwajibika kwa kamati moja ya PAC.

Dk Kashilillah alisema sababu nyingine ni kuangalia utendaji katika baadhi ya nchi, ambazo alisisitiza kuwa hazina kamati za mashirika ya umma.

Mwandishi aliwasiliana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), ambayo iliweka wazi kuwa hakuna sheria yoyote inayozuia mtu kutoa namba ya simu ya mwingine kwa mtu au watu wengine, bila ridhaa ya mwenye namba ya simu.
Ofisa wa TCRA, ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu si msemaji wa taasisi hiyo, alisema sheria ya kuzuia utoaji namba na taarifa za mtu mwingine, inakataza kampuni za simu kufanya hivyo, lakini haizungumzi kwa mtu binafsi. Ofisa huyo alinukuu sheria hiyo:
Taarifa ni siri ya mtu husika, isipokuwa kama mtu huyo ameitoa kwa ridhaa yake.
Alisema pamoja na kuwapo na kipengele hicho, mtu yeyote ambaye ana namba ya simu ya mtu mwingine, hazuiwi kutoa namba hiyo kwa watu wengine.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya   wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, wamesema ingawa namba za simu za viongozi hao zinaweza zikapatikana kwa kila mtu, kuzigawa katika mkutano huo ambao ulikuwa na mtazamo hasi kwa Spika na Naibu wake,  kulikuwa na nia mbaya.
Kama ungekuwa mkutano au semina yenye nia njema na Spika, ungesema wamegawa simu kwa nia njema. Lakini mkutano huo ulivyokuwa na kauli mbovu kwa Spika na taasisi ya Bunge, kitendo cha kuwapa watu namba kinamaanisha walitaka hao watu wamtukane pia.

katika mkutano kama huo, kunakuwa na watu wa kila aina wakiwamo wasio na busara. Hivyo viongozi hao wa CHADEMA waliofanya hivyo, wameshindwa kutumia busara.
Mjumbe wa NEC, Juma Killimbah, ambaye aliwahi kuwa Mbunge na kuhadharisha wananchi wasije kujikuta katika mkono wa sheria kwa kutumia namba hizo vibaya kwa kutoa matusi, alisema simu ya kiongozi huyo kujulikana si ajabu na ni jambo la kawaida.
Tatizo ni maudhui. Kama kitendo hicho kina lengo zuri hakuna tatizo.
Shemu ya taarifa hii imenukuliwa kutoka kwenye gazeti la HabariLeo.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate