EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, February 10, 2013

Taarifa ya Polisi kuhusu Mwanamke aliyefariki akiwa na dawa za kulevya

Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Margaret Temu (45) amekufa ghafla  baada ya kudhuriwa na pipi 64  za dawa za kulevya  alizomeza ili kuzisafirisha kwenda Osaka, nchini Japan akiwa na mwenzake.

Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Viwanja vya Ndege nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)  Deusdedit Kato alibainisha hayo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo.

Kamanda Kato alisema tukio hilo lilitokana na kukamatwa kwa watu wawili kwenye Uwanja wa Ndege  wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakiwa  katika harakati za  kusafirisha nje ya nchi dawa ambazo wanahisi kuwa ni za kulevya katika tukio lililotokea  Jumatano ya wiki hii.

Kamanda Kato alisema  Margaret akiwa na mwenzake Allen Habibu Ally  (28) mkazi wa Tegeta jijini Dar es Salaam walikamatwa na askari wa kike wa Kikosi cha Viwanja vya Ndege nchini (ambaye hakumtaja)  baada ya kuwatilia mashaka.

Kwa mujibu wa Kamanda Kato  askari huyo  alimtilia shaka Ally  na  ndipo alimfuata  na kuzungumza naye  ambapo  baada ya mtuhumiwa kubaini kuwa alikuwa ni askari alimshawishi apokee dola za Marekani 3,000 ili amwachie aendelee  na safari yake  ya Osaka, Japan.

Alisema  askari huyo wa kike (ambaye jina lake limehifadhiwa kutokana  na taratibu za kazi zake) alikataa ushawishi huo na kuamua kuwakamata  Ally na Margret  baada ya kubaini  kuwa  mienendo yao kiwanjani hapo ilionekana kuwa wanafahamiana na wako katika safari moja.
Baada ya kukamatwa Margret na Ally, Polisi waliwahoji na Ally alikiri kumeza  pipi  75 za dawa hizo ambazo zinadhaniwa kuwa  ni za kulevya   lakini Margret alikataa katakata kumeza chochote  lakini  ghafla wakati mahojiano yakiendelea mtuhumiwa huyo alianza kutokwa na damu puani na povu mdomoni na wakati huo huo Ally pia alianza kutokwa na povu
Alisema kitendo hicho kiliwafanya polisi kuwakimbiza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu lakini Margret  alifariki kabla ya kufika hospitali wakati Ally alisalimika  baada ya kupatiwa matibabu.
Baada ya mwili wa Maragret  kufanyiwa uchunguzi na upasuaji mbele ya ndugu zake ambao polisi iliwapata kwa msaada wa maelezo yake yaliyokuwa kwenye  hati yake ya kusafiri alikutwa amemeza pipi 64.
Alisema kwa upande wake Ally, mara baada ya hali yake kutengemaa siku iliyofuata  alirudishwa Polisi ambako alitoa pipi 69  kwa njia ya haja kubwa ambazo polisi wanadhani ndizo alizomeza. Alisema pipi hizo zimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kubaini ni aina gani ya dawa za kulevya.

 Aidha kutokana  na kufanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao na dawa hizo pamoja kugoma kushawishika  kuchukua hongo na kuonesha uadilifu  na uaminifu katika kazi yake, Kamanda Kato alisema Jeshi la Polisi limemzawadia askari huyo Shilingi milioni 5 ambazo ni sawa na kiasi cha dola za Marekani 3,000 ambazo aliikuwa anahongwa na watuhumiwa aliowakamata.

Kwa mujibu wa Kamanda Kato, kuwazawadia askari wa aina hiyo ni sera ya Jeshi la Polisi nchini  ambayo inaelekeza kutoa kiasi hicho  cha fedha kwa askari endapo inathibitika kweli alitaka kuhongwa na kuwataka askari wengine waige mfano bora ulioneshwa na mwenzao.
via HabariLeo

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate