Tunapojiandaa
kuelekea siku hiyo, si vibaya tukakumbushana mambo ya msingi ambayo
yatakufanya wewe na umpendaye muiadhimishe kwa uhuru. Katika siku za
hivi karibuni, marafiki wengi wamekuwa wakinitumia ujumbe mfupi wa
maneno na kunilalamikia jinsi wapenzi wao wanavyowanyanyasa kupitia simu
zao.
Dada Irene wa Sinza, Dar aliniandikia kuwa mpenzi wake amekuwa na kawaida ya kuweka password kwenye simu yake kiasi kwamba hata akitaka kuigusa simu ya mpenzi wake, hawezi kufanya hivyo kwani hukataa kabisa kumtajia namba ya siri.
Akazidi kufunguka kuwa kibaya zaidi, mpenzi
wake anapopigiwa simu wakiwa pamoja, hutoka na kwenda kuzungumza bafuni
au nje kabisa huku akitumia sauti ya kunong’ona. Akaomba ushauri juu ya
tafsiri ya tabia hiyo ya mpenzi wake.Dada Irene wa Sinza, Dar aliniandikia kuwa mpenzi wake amekuwa na kawaida ya kuweka password kwenye simu yake kiasi kwamba hata akitaka kuigusa simu ya mpenzi wake, hawezi kufanya hivyo kwani hukataa kabisa kumtajia namba ya siri.
Kaka Bariki kutoka Sumbawanga yeye alinitumia ujumbe na kunieleza kuwa mpenzi wake huwa anafuta meseji kwenye simu yake kila zinapoingia au anapotuma, wakati mwingine hubakiza zile alizomtumia yeye tu. Kama hiyo haitoshi, pia hufuta hata rekodi za simu zilizoingia au kutoka kwenye simu ya mpenzi wake.
Marafiki,
hao ni baadhi tu ya wengi walionitumia ujumbe lakini wanawakilisha
jamii yetu tunayoishi. Ni ukweli usiopingika kuwa matumizi ya simu
yamerahisisha sana usaliti kwa wapenzi wasiojitambua. Simu zimefanya iwe
rahisi mtu kutoka nje ya uhusiano wake na kulisaliti penzi lake.
Watoto
wa mjini siku hizi wanakwambia ukishapata namba ya simu ya mwanaume au
mwanamke ‘unayemtaka’, basi kila kitu kimeisha. Mipango yote hufanyika
kwa SMS au wakati mwingine kupigiana, appointment hupangwa na mwisho
wawili hukutana na kuvunja amri ya sita.
Walioachana kwa sababu ya
simu ni wengi lakini pia wale ambao wanatifuana kila kukicha, kila mmoja
akimfikiria mwenzake tofauti kuhusiana na matumizi mabaya ya simu idadi
ni kubwa kuliko maelezo.
Leo nataka kuzungumzia kitu ambacho
naweza kutofautiana na wengi lakini ndiyo ukweli hasa katika kipindi
hiki, lengo ni kuleta amani na kuwafanya wapenzi na wanandoa kudumu kwa
muda mrefu bila migogoro. Ninachotaka kusema ni kwamba mnapokuwa katika
uhusiano kisha mkafikia hatua ya kufikiriana ndivyo sivyo kwa sababu tu
ya simu zenu za mkononi ni hatari sana.
Kwa nini mpenzi wako afikie
hatua ya kufikiria kwamba unamsaliti? Inawezekana ni kwa sababu ya namna
unavyompa uhuru wa kuishika simu yako na kufanya anachokitaka. Kwa nini
uweke password ambayo mpenzi wako haijui? Kwa nini ukazungumze na simu
nje? Kuna kipi ambacho hutaki mpenzi wako akifahamu? Hizo ni tabia
zilizopitwa na wakati.
Wapo wapenzi wachache ambao ni mfano mzuri wa
kuigwa, yaani unakuta mtu anamuachia mpenzi wake simu hata kutwa nzima
na anakuwa huru kabisa! Anafanya hivi kwa sababu anajiamini kuwa hana
nyendo chafu na hamsaliti mpenzi wake. Itapendeza kila mmoja akiwa
muaminifu kwa mpenzi wake hasa katika zama hizi zilizojaa maradhi sugu
ikiwemo Ukimwi.
Ukimpa mpenzi wako uhuru kwenye simu yako, bila shaka hamtakwaruzana na mtasherehekea Valentine’s Day kwa mahaba ya dhati.
Ukimpa mpenzi wako uhuru kwenye simu yako, bila shaka hamtakwaruzana na mtasherehekea Valentine’s Day kwa mahaba ya dhati.
No comments:
Post a Comment