EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, February 11, 2013

Wachezaji wa Toto waazima viatu

BAADHI ya wachezaji wa timu ya soka ya Toto Africans ya jijini Mwanza, juzi walilazimika kuingia katika mitaa ya jiji hilo ili kuazima viatu kabla ya mechi yao ya Ligi Kuu dhidi ya Coastal Union iliyofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Hali hiyo ilisababisha mechi hiyo ichelewe kuanza kwa muda wa dakika tano ili kuwasubiri wachezaji ambao walikuwa wameingia mitaani kwa ajili ya kutafuta viatu.

Akizungumza  jana, kocha mkuu wa timu hiyo, John Tegete alisema kuwa wachezaji hao walifikia uamuzi huo baada ya kuhofia kushindwa kucheza vizuri katika mechi hiyo, kutokana na viatu vyao wanavyomiliki kutokuwa na uwezo wa kuhimili matope yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha jijini humo kabla ya kuanza kwa mchezo huo.Alisema hali hiyo yote inachangiwa pia na ukata mkubwa unaoikabili timu hiyo pekee kutoka katika jiji hilo la Mwanza lenye utajiri mkubwa na watu wengi wenye uwezo wa kuisaidia timu hiyo.

“Hakika sikufurahia kabisa hali hiyo, lakini nilishindwa, nifanyeje kwa sababu tunahitaji ushindi ili tuweze kujiweka katika mazingira mazuri ya kuepukana na balaa la kushuka daraja,” alisema Tegete.


Alisema, “Ilibidi niwaruhusu wakaingia mitaani kutafuta viatu, hata hivyo nawashukuru sana vijana wangu waliweza kupambana hadi dakika ya mwisho na bila ya kufungwa na timu ambayo wachezaji wake wanahudumiwa kila kitu na wamekuja Mwanza kwa usafiri wa ndege.”

Katika hatua nyingine, Tegete aliongeza kuwa pamoja na matatizo yote yanayoikabili timu hiyo, hana mpango wowote wa kuachana nayo ispokuwa ataendelea kuiongoza hadi dakika ya mwisho.

Tegete amewataka watu wote wenye mapenzi mema na timu hiyo kujitokeza na kuisaidia ili iweze kukabiliana na changamoto hizo ili kuhakikisha wanapigana na kuendelea kubakia katika Ligi Kuu.

Katika miaka ya hivi karibuni Toto Africans imekuwa ikakabiliwa na ukata mkubwa hali ambayo mara kwa mara imeifanya timu hiyo kuwa na wakati mgumu na kushindwa kutatua matatizo yanayoikabili.

Hivi sasa timu hiyo inashika nafasi ya 12 katika msimo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 13 baada ya kucheza mechi 16, ambapo imeshinda mechi mbili imetoka sare mechi saba na imepoteza mechi saba.    

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate