SHIRIKA la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO),
limekiri kuwapo kwa tatizo la ukosefu wa maji katika baadhi ya maeneo
jijini Dar es Salaam tangu Machi mosi mwaka huu na kuahidi kulifanyika
kazi.
Kauli hiyo ilitolewa na msemaji wa shirika hilo, Irene Makene,
alipozungumza kuhusiana na kero ya ukosefu wa maji
katika baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam.
“Tatizo hilo lipo kweli tangu Machi moja na kuhusu maji kuwa na rangi
mbaya tayari tulishatuma wataalamu wetu kwa ajili ya kuchukua sampuli,
ili tujue tatizo ni nini. Ninachoomba tu ni wakazi wa Jiji la Dar es
Salaam wawe wavumilivu,” alisema.
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wamelalamikia tatizo la
ukosefu wa maji huku shirika hilo likikaa kimya bila kutoa taarifa kwa
wananchi.
Mmoja wa wakazi hao, Jamal Twaha, alisema kinachowakera zaidi ni
shirika hilo kutotoa taarifa yoyote kwa wananchi kwamba kutakuwa na
tatizo la maji.
“Mbaya zaidi hata maji yanapotoka huwa ni machafu ambayo yanahatarisha
maisha ya watu kwani kwa jinsi yalivyo na rangi mbaya ni rahisi kupata
magonjwa ya mlipuko kama vile homa ya matumbo, kuhara na hata
kipindupindu,” alisema.
No comments:
Post a Comment