EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, March 7, 2013

NI KWELI JB AMESHAANGUKA ‘ON BED’ NA MASTAA HAWA?

Na: Erick Evarist
HUWEZI kumzuia binadamu kusema lolote kupitia kuona au kusikia na ndiyo maana siku zote lawama hapewi mbuzi bali binadamu.
Kumekuwa na maneno ya chini kwa chini kwamba, nguli wa sinema za Bongo, Jacob Stephen Mbura ‘JB’  ‘ametembea’ na maua mazuri ya Bongo Movies, Aunt Ezekiel, Jennifer Kyaka ‘Odama’, Shamsa Ford na Wema Sepetu. Swali ni moja tu, kuna ukweli wowote?
Madai hayo yamekuwa yakisikika sana kiasi kwamba, mara kadhaa mapaparazi wamekuwa wakimuuliza JB ambapo kwa vyovyote vile lazima akane. Si rahisi kusema ‘ni kweli jamani’.
Baadhi ya binadamu huwa hawawezi kuishi na donge moyoni, watafanya kila njia kulifikisha katika jamii, wanapoona kitu, hasa cha siri watapenda wengine wajue kama walivyojua wao.
Hata hivyo, wakati wa kufikisha ujumbe huo hujikuta habari zinavuja na kufika kwenye vyombo vya habari.
KWA NINI AHUSISHWE?
Vigezo kama ukaribu, kushirikiana kazi mbalimbali, kuonekana pamoja sehemu tofauti na mastaa hao wa kike, kutaniana vimekuwa vikisababisha staa huyo anayewakimbiza wenzake kwa mauzo sokoni, ahusishwe nao katika uhusiano wa kimapenzi.
Linapokuja suala la kazi, mara kadhaa tumemuona staa huyo ambaye hufurahia ukimwita Bonge la Bwana amekuwa akishirikiana kwa ukaribu na wakati mwingine picha anazopigwa akiwa na kina Aunt Ezekiel, Odama, Shamsa na Wema ndizo ambazo kwa kiasi kikubwa zimezua utata na kuwafanya watu waanze kuzitafsiri wanavyojua wao.
JB ANASEMAJE?
Katika mahojiano maalum na Amani yaliyofanyika kwa takriban saa moja Machi Mosi, mwaka huu, JB aliwapangua warembo hao mmoja baada ya mwingine na kusema hakuna hata mmoja aliyewahi kutoka naye kimapenzi.
Hata hivyo, alikiri kuwepo kwa minong’ono hiyo huku akisema huwa inavuka mpaka na kumfikia mke wake. Alisema huwa inamuuma sana!

 
“Hawa wasanii wote ni watu ambao nafanya nao kazi za sanaa nje ya hapo hakuna chochote kinachoendelea, zaidi ya yote Odama, Shamsa na Aunt nilihusika kwa sehemu kubwa kuwafundisha sanaa na hata Wema nimetoa mchango mkubwa katika sanaa yake, wananiheshimu sana na mimi nawaheshimu pia.
 
“Niliwafundisha misingi ya sanaa, namna gani wanatakiwa kufanya kazi ili kuliteka soko la filamu, wakanielewa na ndiyo maana wote wamekuwa wakinithamini kama mlezi wao kisanaa,” alisema JB.
 
Aidha, JB alikwenda mbali zaidi na kusema, upendo wa wasanii hao kwake umekuwa mkubwa kwa suala la kibinadamu haswa wanapofanikiwa kisanaa, wanajikuta lazima wamshukuru yeye kwa kuwa aliwaonesha dira.
“Nikupe mfano mzuri. Nakumbuka Shamsa  (Ford) alipojifungua mtoto wake wa kwanza kwa mzazi mwezake, Dickson mimi nilikuwa mtu wa kwanza kupigiwa simu ili kujulishwa badala ya mama yake mzazi.
 
“Wananiheshimu na kunijali kwani nimewapa mwanga katika mafanikio ya kazi zao ambazo kila kukicha wananufaika na matunda ambayo pengine bila mimi wasingeweza kuyapata,” anasema JB na kuendelea:
“Siku moja nilitakiwa kwenda harusini na mke wangu, akasema hana nafasi, lakini akasema ili awe ‘komfotabo’ niende na Shamsha kama mwakilishi wangu.” (JB alitoa simu na kumpigia simu mkewe).
 
JB: Eeeh mama.
Mkewe: Haloo baby.
JB: Eti siku ile uliposema huendi kwenye ile harusi ulichagua niende na nani?
Mkewe: Na Shamsa. JB akakata simu huku akimwambia mwandishi: “Si umesikia mwenyewe?”
KUHUSU YANAYOSEMWA
JB hakusita kuwazungumzia wanaoeneza uvumi ambao yeye ameukanusha na kusema kamwe hawezi kumzuia mtu kuzungumza lakini ukweli utabaki palepale kwamba uhusiano wake na maua hayo mazuri ya Bongo Movies, upo kikazi na hata warembo hao wamekuwa wakimshukuru kila kukicha.
ANA MVUTO!
Ucheshi kwa JB ni miongoni mwa vitu ambavyo vimemfanya apendwe na watu wengi. Mwenyewe hapendi kukasirika, kila wakati hupenda kucheka, kila mtu anavutiwa kuwa naye karibu kitu ambacho kwake haoni tatizo kikubwa anachokipinga ni ukaribu huo kuvuka mipaka.
NDOA YAKE IPO IMARA
Kuthibitisha kuwa yeye si mtu wa kuyumbishwa na mapenzi, Bonge la Bwana alizidi kuweka bayana kuwa yeye mume halali wa ndoa iliyodumu kwa takriban miaka 9 bila kuwa na kwaro zozote na anamshukuru Mungu katika hilo.
“Namshukuru Mungu sana, tangu mwaka 2004 nilipofunga ndoa hadi leo nipo kwenye ndoa na sijawahi kuichukia ndoa yangu katika hali yoyote ile,” alisema JB.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate