Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amezitaka nchi zote
ulimwenguni kufanya juhudi maradufu za kuhakikisha kwamba wanawake
wanapewa haki zao. Akizungumza mjini Geneva kwa mnasaba wa kuwadia siku
ya kimataifa ya wanawake, Navi
Pillay amesema kuwa, nchi zote duniani
zinapaswa kusimama kidete na kukabiliana na ukandamizaji unaofanywa
dhidi ya wanawake duniani.
Akielezea wasiwasi wake kuhusiana na
ukandamizaji dhidi ya wanawake uliofanywa hivi karibuni katika baadhi ya
nchi ulimwenguni, Pillay ameongeza kuwa, viongozi wa serikali pamoja na
wakuu wa vyombo vya mahakama katika nchi mbalimbali duniani wanapaswa
kuonyesha hisia zao zaidi dhidi ya ukandamizaji, udhalilishaji wa
kijinsia na ubakaji dhidi ya wanawake, na kusisitiza kwamba wahalifu
wanapaswa kuchukuliwa hatua kali.
Duru za Kimarekani zimeeleza kuwa,
katika kila dakika mbili, mwanamke mmoja wa Kimarekani hunajisiwa na
zaidi ya nusu ya wahanga wa vitendo hivyo ni wasichana waliokuwa na umri
wa chini ya miaka 17. Siku ya kimataifa ya wanawake huadhimishwa
tarehe 8 Machi ya kila mwaka.
No comments:
Post a Comment