Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) pamoja na campus zake wamemtana Waziri Mkuu wa Denmark, Helle Thorning-Schmidt, wakati wa ziara yake ya kukitembelea chuo hicho.
Wanafunzi hao walimtaka Waziri Mkuu huyo kueleza madhumuni ya misaada mbalimbali inayotolewa na serikali yake nchini ikiwamo ya elimu iwapo inatolewa ili kuinua kiwango cha elimu au la.
Kutolewa kwa hoja hiyo kunafuatia wanafunzi hao kudai kuwa iwapo Serikali ya Denmark ingekuwa ikiisaidia Tanzania katika kuboresha sekta ya elimu, elimu nchini isingedidimia wakitolea mfano wa matokeo mabaya ya mtihani wa kiadato cha nne mwaka jana.
Schmidt alisema kuwa serikali yake imekuwa ikiisaidia Tanzania katika sekta ya elimu kwa muda mrefu, lakini kwa sehemu kubwa ilikuwa ikilenga wanafunzi wa elimu ya juu wakiwamo wale wanaochukua shahada za uzamili kwa kutoa ufadhili na ujenzi wa miundombinu katika chuo hicho.
Katika mkutano huo uliojumuisha jumuiya ya chuo hicho, Schmidt alisisitiza umuhimu wa elimu akisema kwamba ni ufunguo wa maendeleo ya uchumi kwa taifa lolote duniani.
Alisema nchi husika inapaswa kuwa na mipango ya makusudi na ya muda mrefu katika eneo la elimu huku akisisitiza kupiga vita mimba kwa watoto wa shule ili kundi hilo liweze kupatiwa elimu kwa kiwango kikubwa kama ilivyo kwa watoto wa kiume.
Soma zaidi: NIPASHE

No comments:
Post a Comment