STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amenusurika kufa ajalini baada ya gari lake kugongana na gari lingine.
Kwenye ajali hiyo, gari la Wolper lilibondeka mbele na kuvunjika kioo cha pembeni (side mirror).
Wolper.
Akizungumza na mwandishi wetu, Wolper alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kumshukuru Mungu kwa kumnusuru kwani hakuumia popote.
“Nilikuwa na mdogo wangu tunaelekea gereji kufuata gari langu, hili nililopata nalo ajali, siyo la kwangu hata sijui itakuwaje!” alisema Wolper.
Hartman Mbilinyi.
Wakati huohuo, Hartman Mbilinyi ambaye ni prodyuza wa filamu, Jumatatu usiku alipata ajali baada ya gari lake kugongana na pikipiki wakati akirudi nyumbani kwake, Tegeta.
No comments:
Post a Comment