KLABU ya Arsenal imerejea katika nafasi
ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England, kufuatia ushindi wa bao
1-0 dhidi ya Fulham kwenye Uwanja wa Craven Cottage katika mchezo ambao
kila timu ilipoteza mchezaji mmoja kwa kadi nyekundu.
Fulham wanaweza kujihesabu hawakuwa na
bahati kwa kushindwa japo kuondoka na pointi moja kwenye mechi hiyo
baada ya kutolewa mapema kwa kiungo Steve Sidwell - ambaye alikuwa
anarejea uwanjani baada ya kumaliza adhabu ya mechi tatu kwa kumchezea
rafu Mikel Arteta dakika ya 12.
Kitu nyavuni: Beki wa Arsenal, Per Mertesacker akiteleza kufunga kwa kichwa
Arsenal ilitumia mwanya huo kujipatia
bao pekee la ushindi dakika ya 43 lililotiwa kimiani na beki Per
Mertesacker kwa kichwa kabla ya Olivier Giroud kutolewa nje kwa kadi
nyekundu dakika ya 90 kwa kumchezea rafu Stanislav Manolev.
Katika mchezo huo, kikosi cha Arsenal
kilikuwa: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Monreal,
Rosicky/Podolski dk71, Arteta, Ramsey, Walcott/Wilshere dk71, Giroud na
Cazorla/Vermaelen dk90.
Fulham: Schwarzer, Manolev, Senderos,
Hangeland, Richardson, Emanuelson/Frei dk87, Sidwell, Enoh,
Kacaniklic/Petric dk85, Ruiz na Berbatov.
No comments:
Post a Comment