WAKATI Ligi Kuu Tanzania Bara ikielekea ukingoni, Kocha Mkuu wa
Simba, Patrick Liewig, tayari ametoa mapendekezo ya wachezaji
watakaobaki Msimbazi.
Kocha huyo alijiunga na klabu hiyo katikati ya msimu huu akichukua mikoba ya Mserbia, Milovan Cirkovic, aliyetimuliwa.
Akizungumza
na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa timu hiyo, Ezekiel Kamwaga,
alisema wachezaji wengi waliopendekezwa na Liewig ni vijana.
“Ni
mapema kuzungumzia usajili katika kipindi hiki, lakini kikubwa ni kwamba
kocha tayari amekabidhi orodha ya wachezaji anaowahitaji watakaoendelea
kuichezea Simba katika msimu ujao.
“Wachezaji hao aliowapendekeza wengi wao ni vijana tuliowapandisha msimu huu na wachache wa timu ya wakubwa ambao amepanga kuwaandaa zaidi,” alisema Kamwaga.
“Wachezaji hao aliowapendekeza wengi wao ni vijana tuliowapandisha msimu huu na wachache wa timu ya wakubwa ambao amepanga kuwaandaa zaidi,” alisema Kamwaga.
No comments:
Post a Comment