BARAZA la Madiwani Wilaya ya Kyela, mkoani Mbeya, limepiga
kura ya kutokuwa na imani na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri hiyo
Abdallah Mfaume kutokana na tuhuma za kutoa zabuni ya ujenzi wa daraja
la Lusungo kwa kamapuni hewa.
Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya, Gabriel Kipija, alisema
halmashauri hiyo ilitangaza zabuni ya ujenzi wa daraja na kampuni
zilizoshindaniwa ni tano na kampuni iliyopita ni Ms China International
Construction Campany ambayo ilipendekezwa na mkoa. Alisema kuwa baada
ya kampuni hiyo kupita, mkurugenzi alipitisha kampuni ambayo
haikuchaguliwa na mkoa ambayo ni Ms CMG Construction Company Limited ya
jiji Mwanza kinyume na taratibu.
Alisema baada ya minomg’ono kutawala mitaani kwamba madiwani
wamehusika kupokea rushwa, ili kupitisha kampuni isiyo na sifa, baraza
hilo liliunda tume ya uchunguzi na kubaini kuwa kampuni hiyo ya Mwanza
imepewa zabuni kujenga daraja hilo wakati mkoa uliipitisha kampuni ya
China kutoka Dar es es Salaam.
Hata hivyo, mwenyikiti alisema licha ya kubaini hilo waliamua kusafiri
hadi Dar es Salaam PPRA kuchunguza uhalali wa kampuni hiyo na kubainika
kuwa kampuni hiyo haipo ndipo walipoitisha kikao cha kamati ya fedha,
ili kuitisha kikao cha dharura. Baada ya kikao hicho, madiwani 24
walipiga kura ya kutokuwa na imani na mkurugenzi na madiwani wanne
walipiga kura ya kuwa na imani na mkurugenzi huyo wakidai kuwa tatizo la
daraja hilo lilikuwepo tangu wakati wa mkurugenzi aliyeondoka, Sinyagwa
Mhando.
Akizungumzia tuhuma hizo, Mfaume alizipinga na kusema kwanza kikao hicho ni batili, kwani wamefanya kinyume na kanuni.
Alisema endepo kuna tuhuma hizo, mwenyekiti alipaswa kupeleka taarifa
kwa mkuu wa wilaya na kisha kwa mkuu wa mkoa ambaye angeunda tume ya
kumchunguza, lakini si kama alivyofanya.
“Hizi ni chuki binafsi za mwenyekiti wa halmashauri dhidi yangu na hii
ni baada ya bodi ya zabuni kuikataa kampuni ya Ms China Charging
Instruction Construction Campanies ya kujenga daraja hilo ambayo hata
hivyo ilionyesha kupigiwa debe na timu ya tathmini ya mkoa ilionyesha
dhahiri mwenyekiti alikuwa na maslahi nayo,” alisema.
Alisema baada ya serikali kutoa fedha za kujenga daraja hilo, bodi ya
zabuni ya wilaya ilitangaza zabuni na makampuni yaliyoomba yalikuwa
matano lakini matatu yaliondolewa na kubaki mawili.
Alisema baada ya kubaki kampuni ya Kichina na kampuni kutoka Mwanza
ndipo mvutano ulipoanza kati timu ya tathmini kutoka mkoani na bodi ya
zabuni ya wilaya ikipendeza kampuni yake.
Mkurugenzi huyo alisema baada ya kuona mvutano huo kumuandikia Ofisa
Mtendaji Mkuu wa PPRA Makao Mkuu, Dar es Salaam, kwa ajili ya kutolea
maamuzi, lakini majibu hayajatolewa ameshangaa kuhusishwa na tuhuma
hizo.
Hata hivyo, mkurugenzi huyo alibainisha baadhi ya sababu za bodi ya
zabuni ya wilaya kuikataa kampuni ya Kichina ni kwamba kampuni hiyo
ndiyo inayolalamikiwa kutengeza barabara za jiji Mbeya iliyofadhiliwa
na Benki ya Dunia chini ya kiwango na kuwa barabara hizo zinatakiwa
kujengwa tena kwa mara pili.
No comments:
Post a Comment